AKAMATWA NA KITITA CHA FEDHA BANDIA JIJINI MWANZA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi
Imeandaliwa na 102.5 Lake Fm
Polisi mkoa
wa Mwanza wanamshikilia mkazi mmoja wa Mtaa wa Machinjioni Kata ya Kata ya
Mahina Jijini Mwanza, kwa tuhuma za kukutwa na fedha bandia zaidi ya shilingi
Milioni Moja na Laki Tano.
Kaimu
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Augustino Nsenga, amemtaja mtu huyo kuwa ni Yohana
Mkalula (42), ambaye alikamatwa baada ya raia mwema kutoa taarifa polisi baada
ya kugundua kwamba fedha alizokuwa nazo si halali.
Inadaiwa
kwamba juzi majira ya saa moja jioni katika eneo la Machinjioni Igoma, Mkalula alifika
kwenye duka na kutoa fedha noti nne za shilingi elfu kumi kila moja ili awekewe
kwenye simu yake kwa kutumia M-Pesa na kabla ya kupewa huduma hiyo mwenye duka
aligundua fedha hizo ni bandia na kutoa taarifa polisi ambapo askari walifika
kwa wakati na kumkamata.
Alipopekuliwa
alikutwa na kiasi cha shilingi Milioni Moja na Laki Tano na hivyo kufanya jumla
ya fedha bandia alizokamatwa nazo kuwa shilingi Milioni Moja, Laki Tano na Elfu
Arobaini ambapo mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa kabla ya kufikishwa
mahakamani.
Kaimu Kamanda Senga amebainisha kwamba msako mkali unafanyika
ili kubaini watuhumiwa wengine wanaohusika na mtandao wa utengenezaji wa fedha
bandia ambapo ametoa rai kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza kutojihusisha na shughuli
za kiuhalifu na badala yake wajikite kwenye shughuli halali na za kimaendeleo
ili kuepuka kutiwa nguvuni na polisi.
No comments: