LIVE STREAM ADS

Header Ads

BARAZA LA HABARI NCHINI LABAINI HASARA KWA MATANGAZO YA BUNGE KUTOONEWA "LIVE".

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Uchunguzi  uliofanywa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kuhusu kuzuiwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za bunge umebaini kuwepo hasara za uamuzi huo.

Hayo yamebainishwa jana Jiji Dar es salaam kwenye uzinduzi wa ripoti ya bunge iliyozinduliwa na MCT iliyobainisha kwamba ni hasara kubwa wananchi kunyimwa fursa ya kufuatilia taarifa za moja kwa moja za matangazo ya bunge.

Mwenyekiti wa tume za haki za binadamu  na utawala bora,  Bahame Nyanduga, alisema matangazo ya bunge yangeweza kuendelea kwa kugharamiwa na vyanzo visivyo vya serikali tofauti na ilivyoelezwa kwamba yamesitishwa kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa.

Aidha amesema  taarifa hii inaweza kusaidia viongozi wanaohusika na maamuzi hayo kuona ni jinsi gani uhuru wa maoni ni muhimu kuliko gharama.

No comments:

Powered by Blogger.