LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC SENGEREMA MKOANI MWANZA APIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA BODABODA USIKU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha bodaboda mkoani Mwanza, Makoye Kayanda.
Na BMG
Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uhalifu ikiwemo unyang’anyi na mauaji kwa kutumia pikipiki katika Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Mkuu wa Wilaya hiyo Emmanuel Kipole, amepiga marufuku waendesha bodaboda wilayani humo kufanya kazi nyakati za usiku.

Taarifa ya zuio hilo ambayo tayari imewasilishwa kwa Umoja wa Waendesha bodaboda wilayani Sengerema, imezuia matumizi yote ya pikipiki kuanzia majira ya saa sita na dakika thelathini usiku hadi saa kumi na moja kamili alfajiri hadi pale zuio hilo litakapositishwa. Taarifa ya zuio hilo ilitolewa juzi Oktoba 28 mwaka huu.

Akizungumza na 102.5 Lake Fm Mwanza, Mwenyekiti wa Umoja wa Waendesha bodaboda mkoani Mwanza, Makoye Kayanda, amesema zuio hilo si suluhisho la uharifu hadi pale shughuli nyingine za kibiashara zinazofanyika usiku zitakapozuiliwa.

Aidha Kayanda amesema ni vyema ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema ikashirikiana na waendesha bodaboda katika kuimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo husika ikiwemo kuwasajili waendesha bodaboda wanaofanya kazi nyakati za usiku.

No comments:

Powered by Blogger.