EDWIN SOKO: WAANDISHI WA TANZANIA TUMEKUWA WAZITO KUTAFUTA FURSA ZA KIMATAIFA ILI KUJIFUNZA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na Edwin Soko
MKUTANO wa The African Investigative Journalism umemalizika kwa Mwaka 2016 umemalizika mapema wiki hii, kwenye chuo kikuu cha Wits hapa Johannesburg Afrika ya Kusini na kuhudhuriwa na mamia ya Waandishi wa Habari.
Mfuko wa Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania(TMF) ulibeba jukumu kubwa na kuitoa Tanzania kuwa mtazamaji hadi kuwa mshiriki wa mkutano huo, kwa kuwawezesha Waandishi wa Habari wanne kuhudhuria mkutano huo.
Nikiwa kama mmoja kati ya washiriki wa mkutano huo kuna mengi nimejifunza kwa muda wasiku tatu kuanzia Novemba 7 hadi 9 mwaka huu, kwa utashi, uelewa na kutokuwa na roho ya ubinafsi, naomba ruhusa yenu kuyaleta machache mbele yenu Waandishi wenzangu ili tuweze kunufaika wote.
Tanzania ina kazi nyingi zenye vigezo zikiwemo zile zilizotengenezwa chini ya miradi ya TMF lakini Waandishi tumekuwa hatuziwakilishi kwenye majukwaa ya kimataifa ili kazi zetu ziweze kutambulika na matokeo yake tumekuwa tukiwaacha Waandishi wa mataifa mengine wakitamba kwenye medali za kimataifa na kujulikana kwa kazi zao na kupata heshima kubwa.
Nani asiyemjua Mohamed Ali, Mwandhishi mpekuzi wa kituo cha KTN, kazi za waandishi wetu kama zilizoibua ufisadi wa bandarini, scandal ya Escrow na sumu ya sayanaidi kwenye mto Tegeta, ziko wapi?
Tumeshuhudia kazi zilizofanywa na Waandishi mbali mbali zikiwakilishwa mfano Ile ya kashifa ya rushwa kwenye michuano ya Olympic Reo de Jenairo na Ile ya Panama paper zikitamba kweli kweli.
Napenda kuwakumbusha kuwa, siku zote usipojikubali mwenyewe kabla mwingine hajakukubali, naomba tulitafakari jambo hili ndugu zangu waandishi.
Waadishi wa Tanzania tumekuwa wazito wa kutafuta fursa za kimataifa ili kujifunza, kuonyesha na kujijenga kiuwezo wa kitaaluma, tumekuwa tunaacha majukwaa mengi ya kitasnia yakifanyika bila Kuwa na uwakilishi wa Nchi.
Najua wengi tutasema ni uwezo mdogo wa kifedha, lakini si kwelichanzo kikubwa ni kutoona fursa mbele yenu na kutaka tuwe wakina nani kwenye kujivunia tasnia yetuMwandishi wa upekuzi wa Kenya Mohamed Ali toka kituo cha KTN alinena na mimi na kuniambia kuwa , anashangaa kuona angalau watanzania kwenye mkutano huu tofauti na mikutano mingine ya kimataifa, kwa kweli niliumia sana nikabaki naugulia moyoni.
Nikataka kujua mataifa mengine inakuwaje?Hapo nilibaini Kuwa, wenzetu wanafanya sana mikakati ya kifursa na mahusiano ( lobbying na connections development) ili kuweza kujichanganya na ulimwengu wa pamoja , wakati sisi tunajifungia milango kwa kuamini tunachokifanya ndicho sahihi, wakati kumbe tunajimaliza wenyewe, nina imani kila Mwandishi mmoja mmoja akaanza kufungua mahusiano na kuwa na jicho la mbali la kutaka mafanikio kwenye tasnia kupitia dunia Kijiji tunaweza kuiendeleza tasnia ya habari Tanzania,hali hii ni tofauti na wenzetu hawapotezi hata dakika kwenye fursa.
Vyuo vya kitaaluma na taasisi za kitaaluma vinawajibu wa kuileta tasnia kwenye kijiji kimoja, lakini huku nyumbani wajibu wa vyombo hivyo ni mdogo sana na havifanyi advantages analysis ya Kuwa host wa mikutano mikubwa ya kitasnia, ni jambo hili linajidhihirisha toka kwenye mkutano huo mkubwa kutoona uwakilishi wa taasisi za kihabari tofauti na TMF, lakini kwa Nchi nyingine uwakilishi wa kitaasisi ni mkubwa mno na ndio unaohamsha hamasa.
Mfano mkutano ulioisha hapa Wits university umekibeba chuo kwa kutangaza kitivo cha mawasiliano ya umma, washiriki wengi tumeonyesha nia ya kutaka kusoma chuoni hapo, huo ndio mikakati ya taasisi za kitaaluma kwenye kutafuta fursa, lakini hapo kwetu Nyumbani naona vyuo vingi vinajitangaza kwa kutumia Vyombo vya habari tena kwa kulipia, dunia imegeuka wenzetu wanajitangaza kwa kuleta fursa na wakati watu wanachangamkia fursa na wao wanageuza watu hao kuwa fursa za kitaaluma.
Faida nyingine kwa vyuo vya kitaaluma ni kuwajenga wanafunzi wao kitaaluma, Kuazia mkutano uanze November 7 hadi 9 wanafunzi wote wa kitivo cha mawasiliano ya umma kuanzia degree hadi PhD walikuwa wakishiriki matukio mbali mbali pamoja na kutafuta fursa za connections development, je wanafunzi toka kwenye vyuo vyetu wataweza kweli kushindana na wanafunzi kama wa Witz waliojengwa kisaikolojia na kimahusiano ya kidunia?
Kwa kuwa sasa tasnia ya habari inakwenda kurasimishwa kuwa taaluma ni vyema tukajifunza toka kwa wenzetu ili nasi tuweze kupiga hatua, natamani kuona mkutano ujao kazi za Waandishi toka Tanzania zinatangazwa na kujulikana kimtaifa, tumechoka kuona wenzetu wakimilki tasnia ya habari, ebu tujaribu mbona bongo movie wameweza kila kitu ni kupanga tu na kutia nia.Kwa kupitia fursa niliyoipata toka TMF nimejifunza mengi na nimeona bora niandiko andiko hili fupi ili nanyi wenzangu mlisome.

Soma HAPA Pia
No comments: