LIVE STREAM ADS

Header Ads

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI JIJINI DAR ES SALAAM KUTOA HUDUMA YA KUPANDIKIZA FIGO.


Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na James Salvatory, BMG Dar
Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2017 itaanza huduma ya upandikizaji figo hapa nchini na kuweza kupanua huduma za kusafisha figo ikiwa na lengo la kutimiza azima ya serikali ya kupunguza idadi ya wagonjwa kwenda nje ya nchi kupata huduma hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha, alisema uwepo wa huduma hiyo hapa nchini utawawezesha watanzania kupata huduma hiyo kwa gharama nafuu zaidi na kuweza kuipunguzia mzigo serikali kwa kupeleka wagonjwa nje ya nchi kutibiwa.

Pia alisema kwa kuzingatia hilo hospital imefanikiwa kupeleka wataalamu wake nje ya nchi kupata ujuzi zaidi ili kupunguza tatizo la upandikizaji figo na kupata ujuzi wa upandikizaji wa kifaa cha usikivu kwa watoto.

Takwimu za hospital hiyo zinaonesha kuwa asilimia 95 ya wagonjwa ambao wanahitaji kufanyiwa upasuaji na kuweza kuwekewa kifaa cha usikivu kwa watoto wadogo kupitia taaluma hiyo waliyopata itawajengea uwezo kwa wataalamu wa ndani ya nchi kufanya huduma hiyo kikamilifu na kuweza kupugunza gharama za kwenda nje.

" Katika kipindi cha mwaka mmoja wa awamu ya tano hospitali imenunua mashine mpya ya CT- Scan yenye uwezo wa 126 slices yenye kiwango kikubwa cha kupima wagonjwa wengi kwa wakati mmoja, tunaweza kumpima mgonjwa mmoja tumbo na kifua kwa sekunde sita" alisema.

Aliongeza kwamba kwa sasa wagonjwa hospitalini hapo wanapata dawa kwa zaidi ya asilimis 96 kwenye maduka ya dawa, pia nakuweza kuongeza vifaa vipya vya kisasa ili kuhakikisha hiduma hiyo inatolewa kwa ubora wa hali ya juu.

No comments:

Powered by Blogger.