LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA ACACIA YAIPIGA TAFU HOSPITALI YA MJI WA KAHAMA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia
Kampuni ya Acacia kupitia mgodi wake wa dhahabu wa Buzwagi, imekabidhi vifaa mbalimbali katika hospitali ya halmashauri ya Mji wa Kahama kwa lengo la kuendelea kuboresha utendaji kazi pamoja na huduma za afya hususani  mama na mtoto.

Vifaa vilivyokabidhiwa katika hospitali hiyo vina thamani ya shilingi milioni 22.4 ambapo Meneja wa mgodi huo Asa Mwaipopo alivikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na mashine tatu za kutengeneza Oxgeni, viti vitano kwa ajili ya kusukumia wagonjwa, machela mbili, mashine mbili maalumu ya umeme ya kusafishia vifaa vya upasuaji pamoja na mashine moja ya upasuaji.

No comments:

Powered by Blogger.