LIVE STREAM ADS

Header Ads

POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM WATOA TAHADHARI KWA WANANCHI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Displaying IMG_20161031_130254.jpg
Na James Salvatory, BMG Dar
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, limewataka wakazi wa Jiji la dar es na wageni Kutoka sehemu mbalimbali kuwa makini na matapeli wanaotumia mbinu za kila aina hususani viongozi wa serikali au watu mashuhuri kujipatia fedha kwa njia za kidanganyifu.

Kamishina wa  polisi kanda hiyo, Simon Sirro, amesema hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa raia wa kigeni kwamba kuna waarifu wanaotumia  vibaya jina la mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kuwataka watoe pesa za kigeni ikiwemo dola za Kimarekani na pesa za Kitanzania kwa madai ya kuwasaidia wanafunzi kupata vyuo nchi za nje.
Displaying IMG_20161031_132216.jpg
Katika hatua nyingine jeshi la polisi kanda hiyo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa  220 kwa tuhuma mbalimbali za kiharifu ikiwemo kucheza kamali, unyanganyi, kubugudhi pamoja na kununua na kuuza gongo.

No comments:

Powered by Blogger.