LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAHAMA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia
Wananchi wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuchangamkia fursa za kibiashara ambazo zitakazotokea hivi karibuni wakati wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda kwenda katika jiji la Tanga litakopopita wilayani hapa.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu, aliyasema hayo wakati akiongea na madiwani wa halmashauri ya Msalala katika kikao maalumu cha baraza la madiwani kilichofanyika mwishoni mwa wiki.

Nkurlu alisema  katika ujenzi wa Bomba hilo la mafuta wanategemea kuwepo kwa zaidi ya ajira 1,000 kwa wakazi wa mji wa Kahama.

No comments:

Powered by Blogger.