LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIRIKILA LA KUHUDUMIA VIWANDA VIDOGO SIDO LAWANOA WATU WENYE ULEMAVU KANDA YA ZIWA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoa wa Mwanza,  limewapatia mafunzo ya ufugaji kuku na utengenezaji wa vikapu,  watu wenye ulemavu  mbalimbali 45, kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Afisa Biashara SIDO mkoa wa Mwanza, Maneno Maporo, alisema mafunzo hayo yameandaliwa na shirika hilo chini ya mradi wake wa Kuwainua Watu Wenye  Ulemavu (EPWDS), yanayafanyika kwa siku 10 ambayo utolewa kila mwaka.

Maporo alisema, washiriki 30 kutoka wilaya za mkoa wa Mwanza wanajifunza ufugaji wa kuku, huku 15 kutoka mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa watapatiwa mafunzo ya utengenezaji wa vikapu.

Alisema, lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha walemavu kujikwamua kiuchumi, kujiajiri na kuacha kuwa tegemezi.

Pia alisema, mafunzo hayo utolewa bure kwa washiriki hao, wenye uhitaji na wapo tayari kupitia viongozi wa vyama vyao, ambao ndio wanawachagua.

Hata hivyo alisema, tangu kuanza kwa mradi huo, walemavu walioshiriki wameweza kujikwamua kiuchumi sambamba na kujiajiri na kuajiri wengine.

Aidha aliwaomba walemavu kuchangamkia fursa zinazojitokeza pamoja na kujishughulisha,ili kujiinua kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi.

"Kuwa mlemavu siyo mwisho wa maisha, kwani wapo wanaofanya vizuri na kujishughulisha wamefanikiwa,hivyo fursa mlionayo ni vizuri mkaitumia ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi, " alisema Maporo.

Vilevile aliiomba, serikali itengeneze mazingira mazuri yatakayo wafanya walemavu waweze kushiriki katika masuala mbalimbali ikiwemo kiuchumi, kiafya na kijamii, kwani SIDO wameona wanaweza.

Kadhalika aliongeza kwa kuomba mashirika na kampuni binafsi kuwawezesha  na kuwekeza kwa walemavu, kama wanavyofanya kwenye burudani, ili waweze kujikwamua kiuchumi.

No comments:

Powered by Blogger.