LIVE STREAM ADS

Header Ads

LICHA YA KULALAMIKIWA NA WADAU, RAIS MAGUFULI ASAINI MUSWADA WA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI 2016.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli, jana ameusaini muswada uliolalamikiwa na wadau wengi wa habari nchini wa Huduma ya Vyombo vya Habari wa mwaka 2016 kuwa sheria kamili. 

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, imeeleza kwamba Rais Magufuli amewapongeza wadau wote waliofanikisha kutungwa kwa sheria hiyo ambayo amesema itasaidia kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma wenyewe na Taifa. 

Huku Mwanza uwanja wa Nyamagana unaelekea ukingoni kumalizika kwenye uwekaji nyasi bandia, nimepita kupiga picha wakati nawaza ikiwa nitapata mkopo ili nikaongeze elimu maana mikopo ya elimu ya juu ni janga la Taifa nchini kwa sasa, je tutasoma?, Nijibu kupitia ukurasa wangu wa Facebook https://www.facebook.com/gbpazzo

Baadhi ya mapungufu yaliyoelezwa na wadau wa habari nchini.
Kwanza, muswada huu unaipa serikali mamlaka makubwa ya kuwabana waandishi wa habari. Hususani, kwa kuanzisha mfumo utakaowataka waandishi wa habari kupata vibali, kupitia Bodi ya Ithibati ya Wanahabari ambayo itakuwa na wajumbe saba. Wajumbe wote watateuliwa na Waziri.

Sheria na taratibu za kimataifa zipo wazi: si halali kutoa vibali kwa waandishi wa habari ama kuweka masharti ya nani anaweza kuwa mwandishi wa habari. Muswada huu ukipirishwa kuw sheria, waandishi wote wa habari hapa nchini watajazwa na hofu yakufanya kazi zao ipasavyo kwa kuogopa kunyang’anywa vibali vyao.

Pili, muswada unataka vyombo vya habari (magazeti) kuwa na leseni. Unaipa serikali mamlaka ya kusimamia utoaji wa leseni hizo. Tatizo kuu la Sheria ya Magazeti (1976) litaendelea kubaki palepale.

Tatu, muswada huu uniangila uhuru wa vyombo vya habari kwa kuweka uwezekano wa kuvilazimisha vyombo vya habari, vikiwemo vyombo binafsi, kutangaza habari kama inavyoelekezwa na serikali.

Nne, vifungu vya muswada vinavyohusika na kauli za kashfa pamoja na uchochezi vinavuka mipaka inayokubalika kwenye nchi za kidemokrasia. Kifungu kimoja, kwa mfano, kinasema kauli iliyochapishwa inaweza kusemekana kuwa ni ya kashfa hata kama kauli hiyo ni ya ukweli. Muswada wa sasa unaainisha kuwa kauli ni lazima iwe ya kweli na “yenye manufaa kwa umma”. Na bila shaka serikali ndiyo itakayoamua kauli ipi “ina manufaa kwa umma.”

Hakuna mtu anayedai kwamba vyombo vya habari hapa Tanzania vimekamilika kimaadili na kitaaluma. Tasnia ya habari nchini inaandamwa na matatizo ya upendeleo, usahihi wa habari, rushwa na uongo wa kupindukia. Kuna utofauti kubwa kati ya Marekani ya mwaka 1801 na Tanzania ya mwaka 2016, lakini malalamiko mengi ya Thomas Jefferson kuhusu magazeti ya Marekani miaka mia mbili iliyopita yana uhalisia hapa nchini Tanzania.

Lakini, jawabu la Jefferson halikuwa kutunga sheria zenye lengo la kuubana uhuru wa magazeti yaliyomkera. Hili linapaswa pia kuepukwa nchini Tanzania. Vyombo huru vya habari na vinavyojitegemea ni sehemu muhimu ya serikali ya kidemokrasia inayowajibika.

Muswada huu wa Sheria ya Huduma za Habari ukipita kama ulivyo, utaunyonga uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania. Utasababisha janga kubwa la “uwepo wa serikali isiyokuwa na magazeti.” Janga hili linaepukika kwa uzalendo na ujasiri wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tujikumbushe wakati bunge linapitisha mswada huo.
Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umepitisha rasmi Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ambapo hatua inayofuata ni kuridhiwa na kusainiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili uwe Sheria kamili ya nchi.

Muswada huo umepitishwa leo Bungeni mjini Dodoma ambapo mkutano huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Andrew Chenge.

Wabunge walijadili Muswada huo kifungu kwa kifungu na kuunga mkono upitishwaji wake baada ya Waziri mwenye dhamana na habari kutoa hoja ili Muswada huo uweze kujadiliwa.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupitishwa Muswada huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amewashukuru wadau wote walioshiriki katika kutoa maoni juu ya Muswada huo kwani ndiyo yamepelekea kukamilisha mchakato mzima wa Muswada huo.

“Kwa niaba ya Serikali napenda kuwashukuru wadau wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuhakikisha tunatimiza malengo ya takribani miaka 20 iliyopita ya kuifanya taaluma hii ya habari kuheshimika kama zilivyo taaluma zingine”, alisema Waziri Nape.

Waziri Nape ameongeza kuwa kwa sasa Muswada huo umeshapitishwa hivyo kilichobaki ni utungaji wa Kanuni ambapo ameomba wadau wa tasnia ya habari kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kutoa maoni yatakayopelekea kuwa na kanuni zenye tija kwa wanahabari na taifa kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Nape amewaasa wadau wa habari kuunganisha nguvu kwa pamoja hasa katika kipindi hiki ambacho Muswada huo umepitishwa pia amewataka wadau hao wasiruhusu mgawanyiko utokee kati yao bali washirikiane na Serikali katika kutekeleza wajibu wao wa kihabari kwa jamii.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ni mwanzo mpya wa tasnia ya habari nchini ambapo amewaasa wadau wa habari wakiwemo waandishi wa habari kutambua kuwa haki mara zote huendana na wajibu, hivyo hakuna haki isiyo na wajibu.

Muswada huo uliopitishwa leo umejadiliwa na Bunge hilo kwa siku mbili ambapo kwa mara ya pili ulisomwa mbele ya Kamati ya Bunge zima na hatimaye kusomwa kwa mara ya tatu ili kukidhi hatua za utungwaji wa sheria nchini.
                   KWA MSAADA WA MITANDAO MBALIMBALI

No comments:

Powered by Blogger.