LIVE STREAM ADS

Header Ads

NCHI ZA MAZIWA MAKUU IKIWEMO TANZANIA ZATAKIWA KUHESHIMU UHURU WA HABARI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying IMG-20161108-WA0016.jpg
Na Edwin  Soko, Johannesburg Afrika Kusini
Nchi za  maziwa  makuu  ikiwemo  Tanzania  zimeaswa  kuheshimu  Uhuru  wa vyombo  vya  habari  na  haki  ya  kupata  taarifa  ili  kuzipa  maendeleo  nchi  zao  na  kuyafikia  maendeleo  endelevu  ya  kidunia  ifikapo  mwaka  2030.

Hayo  yamesemwa na  Mwandishi wa  habari  wa  Burundi, Bob  Rugurika  wa kituo  cha  Radio Publique  Africaine  nchi   Burundi,  anayeishi  uhamishoni  alipokuwa  anatoa  ushuhuda    kwenye  muendelezo  wa mkutano  wa  kimataifa  wa  Afrika  unaofanyika  Jijini Johannesburg, Afrika  ya  Kusini.

Ruganika  amesema  yeye  amelazimika  kuishi  uhamishoni  sio  kwa kupenda  bali ni  kutokana  na  hali  ya  usalama ilivyo  mdogo  nchini Burundi  na  kushuhudia zaidi ya waandishi wa  habari  100  wakishikiliwa   kwenye  Magereza nchini  humo  pamoja  na  kufungwa  kwa  vituo  vyote  vya  kihabari vya  kibinafsi.

“Ndugu  zangu  waandishi  nimenusurika  kufa  mara  kadhaa    Nchini Mwangu  kutokana  na  kazi  yangu  ya  kuonyesha  uminywaji wa haki za binadamu  nchini Burundi, hivi sasa mimi na  familia  yangu  tunaishi  uhamishoni   kwa  ajili  ya  kunusuru  maisha  yetu” Alisema.

Akifanya  mahojiano  na mwandishi wa habari hii, alisema ni  wakati wa muafaka  kwa sasa  nchi za Maziwa  Makuu  kuheshimu  demokrasi  kwa  viongozi  wake  kutojaribu  kupindisha  katiba  za  nchi  na kuendelea  kubaki madarakani.

“Napenda  sana  mfumo wa Tanzania wa kubadilishana  uongozi    kwa  kufuata  misingi  ya  katiba  nafikiri  ndiyo  mfano  pekee  wa  Marais  wengine  kuiga  mwenendo huo” alihitimisha  Ruganika.

Wakati  huo  huo  Mkurugenzi  wa  Wakfu wa Tasinia  ya  Habari Tanzania,  Ernest Sungura  (TMF)  amewataka  waandishi  kutoka  Tanzania  kujifunza  yanayoendelea  kwenye  mkutano  huo ili  waweze  kuwa  mabalozi  mazuri  watakaporudi  nyumbani.

TMF  imekuwa  ikitambua   mchango  wa  kazi  za waandishi wa Tanzania hasa  za  uchunguzi  na  kuamua  kuwapa  nafasi   baadhi  ya  waandishi  waliofanya  kazi  nzuri  kuhudhuria  mkutano  huo  ili  waweze  kuziendeleza  kazi  zao  kwa  ufanisi  zaidi.

Mkutano  huo  unafanyika  kwenye  Chuo  Kikuu  cha  Wits  hapa  Johannesburg  na kutaraji  kumalizika  November  9 mwaka huu.
Soma HAPA Habari ya mwanzo.

No comments:

Powered by Blogger.