LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAFANYABIASHARA WA VIUMBE PORI NCHINI WAOMBA RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying IMG_20161109_102436.jpgNa James Salvatory BMG Dar
Wafanyabiashara wa viumbe pori nchini wamemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli, kuwafungulia biashara yao ya viumbe hai kwenda nje ya nchi baada ya kusitishwa ghafla tangu Machi 17 mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Magembe

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Viumbe pori hai, Salim Mussa, amesema kuwa wanamuomba Rais Magufuli aingilie kati swala hilo na kupata ufumbuzi wa kudumu wa kuendelea na biashara hiyo ya viumbe kwa maendeleo yao na uchumi wa Taifa.

“Tunakuomba Mh.Rais Magufuli uingilie kati swala hili na kutupatia ufumbuzi wa kudumu ili kuendlea na biashara ya viumbe pori hai bila ya usumbufu wa mara kwa mara kwani biashara hii ipo kwa mujibu wa sheria , taratibu na kanuni za nchi” alisema Salim.

Aidha Salim amesema kuwa maamuzi hayo yanaweza kusababisha hasara kubwa kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa viumbe hivyo na uchumi wa nchi kwa ujumla kwani  muongozo haujatolewa tangu kusitishwa kwa biashara hiyo mwezi machi mwaka huu.

Kwa upande wake msemaji wa wafanyabiashara wa viumbe pori hai  Enock Balilemwa, amesema kusitishwa kwa biashara hiyo imepunguza kiwango cha ajira kwa kiasi cha watanzania milioni moja ambao asilimia 95 wanaishi vijijini.

“Kusitishwa kwa biashara hii ya viumbe pori hai imefanya watanzania takribani milioni moja hasa wakazi wa vijini asilimia 95 kukosa ajira jambo ambalo linapelekea wananchi hao kukosa uwezo wa kujikimu kwa maisha ya kila siku” Amesema Balilemwa.

Biashara hiyo ya viumbe pori hai inayojumuisha vyura, wadudu, ndege, mijusi, tumbili, hifadhi za wanyamapori (Zoo) na mashamba ya wanyapori ilianza kabla ya uhuru sambamba na leseni zingine za uwindaji wa kitalii ambayo mpaka sasa inatambulika kwa sheria namba tano ya mwaka 2009.
Displaying IMG_20161109_103917.jpg

No comments:

Powered by Blogger.