LIVE STREAM ADS

Header Ads

NI SHANGWE NA NDEREMO KWA WAFUASI WA RAIS MTEULE WA MAREKANI DONALD TRUMP. MARAIS AFRIKA WAANZA KUMPONGEZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump akizungumza baada ya ushindi.
Hillary Clinton and Donald TrumpMgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump (kulia), ameshinda kiti cha urais wa nchi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana.

Trump ameshinda kwa kupata kura za wajumbe maalum 276 na kupita idadi ya wajumbe 270 iliyotakiwa dhidi ya 218 alizopata mpinzani wake Hillary Clinton wa Democratic (kushoto).

Akizungumza hivi punde, Trump ambaye anakuwa rais wa 45 wa Marekani amewashukuru wafuasi wake na kusema amepigiwa simu na Hillary Clinton na kuwapongeza.

Shangwe, nderemo na vifijo zimetanda miongoni mwa wafuasi wa Donald Trump ambao awali hawakuwa na uhakika kama mgombea huyo angeshinda.

Kwa upande wa kura za wananchi, Trump amepata zaidi ya kura milioni 56 huku Clinton akiwa na kura milioni 54. 
Trump anasubiri kuapishwa ambapo anafanya mazungumzo na wanahabari pamoja na wafuasi wake.
Donald Trump alipakia picha hii kwenye Twitter, yake, mgombea mwenza wake na jamaa na marafiki wakifuatilia matokeo New York.
Picha ya awali, Trump akiwa na mgombea mwenza wake, ndugu, jamaa na marafiki zake wakifuatilia matokeo ya uchaguzi.

Trump ameshinda ngome za Republican katika majimbo ya Alabama, Kentucky, South Carolina, Nebraska, Indiana, West Virginia, Mississippi, Tennessee, Oklahoma, Wisconsin, Alaska, Pennsylvania na Texas.

Naye Clinton ameshinda zaidi ngome za Democratic kwenye majimbo ya New York, New Jersey, Connecticut, Massachusetts, Maryland, Vermont, Delaware, Illinois, Rhode Island na District of Columbia. 
Hillary Clinton
Bi.Clinton ameweka picha hii mtandaoni akiwashukuru watu wote licha ya kushindwa kwenye uchaguzi huo.

MARAIS AFRIKA WAMPONGEZA TRUMP
Rais wa Tanzania John Magufuli ameandika ujumbe kwenye Twitter akimpongeza rais mteule wa Marekani. Ameahidi kwamba Watanzania wataendeleza urafiki na Marekani.

"Congratulation President-Elect and people of America for a democratic election,I assure and people of Tanzania for a continued friendship". @MagufuliJP

Naye Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ni miongoni mwa viongozi waliompongeza Donald Trump kupitia Twitter. Amesema ushindi wa Trump ni ushindi wa Wamarekani wote.

"Mr. @realDonaldTrump, on behalf of the people of Burundi, we warmly congratulate you. Your Victory is the Victory of all Americans". @pnkurunziza
Imeandaliwa na BMG kwa msaada wa mtandao. Tazama HAPA

No comments:

Powered by Blogger.