Mkuu wa mkoa wa Mara afanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani humo.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mkuu wa mkoa wa Mara, Dkt. Charles Mlingwa (kushoto) leo asubuhi amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Mugini Jacob (kulia) katika Hoteli ya Goldland iliyopo mjini Tarime.
Pamoja na mambo mengine, wamekubaliana kufanya kazi kwa karibu katika kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika mkoa wa Mara na kuhamasisha masuala ya maendeleo kwa ujumla.
Fursa za uwekezaji katika mkoa wa Mara zipo katika sekta za mbalimbali ikiwemo Utalii, Madini, Kilimo pamoja na Uvuvi ambapo sasa Mara ni kitovu cha uwekezaji.

Picha na Mtandao wa Mara Online
No comments: