LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA UMOJA WA MATAIFA KUTEKELEZA MALENGO 17 YA MAENDELEO ENDELEVU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Serikali kwa kushirikiana na Umoja wa mataifa (UN), imejipanga kuyashirikisha makundi maalumu katika kutekeleza malengo 17 ya umoja wa mataifa  ya mandeleo endelevu kufikia 2030.

Serikali katika kutekeleza malengo hayo imeamua kuyashirikisha makundi hayo ambayo ni pamoja na Wanawake, walemavu pamoja na watoto katika shughuli za kiuchumi, kijamii pamoja na kisiasa.

Akizungumza jana katika kongamano lililoandaliwa na UN, kwa niaba ya Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Katibu mkuu wa wizara hiyo, Sihaba Nkinga alisema serikali imeandaa mipango maalum ya kuhakikisha nchi inafikia maendeleo endelevu kwa kuyashirikisha makundi maalumu ambayo yalisahaulika tangu nchi ilipopata uhuru.

Alisema kuna haja ya kutambua makundi hayo kwa kujua yanaishi wapi na yanafanya shughuli gani za kiuchumi zinazoweza kufikia maendeleo endelevu na kwamba serikali ipo tayari kuyashirikisha na  kuyawezesha kwa kuyapa elimu ya ujasiriamali.

“Utekelezaji wa maendeleo endelevu utafanikiwa ikiwa  tutayatambua makundi maalum ambayo ni wanawake, walemavu pamoja na wazee tujue wanaishije,wapi na akina nani….serikali ipo tayari kwa kushirikiana na Umoja wa mataifa kuyawezesha makundi haya kwa kuyapa elimu na kuyaweka karibu na taasisi za kifedha,” alisema Nkinga.

Nkinga aliongeza kuwa serikali pamoja na wadau binafsi wanatakiwa kuyatambua na kuyasaidia makundi hayo kwani yakiwezeshwa yataisaidia serikali pamoja na jamii kwa ujumla katika kupambana na umasikini nchini.

Alisema serikali haipo tayari kuona mtu yeyote anaachwa nyuma katika utekelezaji wa maendeleo endelevu na kwamba kila mtu anajukumu la kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii ili kukuza uchumi wa nchi na kwamba wamejipanga kutoa elimu kwa wote hususan ujasiriamali.

Hata hivyo alizungumzia changamoto zilizopo ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto na kwamba jamii iwe tayari kukemea hilo kwani maendeleo hayatafikiwa ikiwa masuala hayo yataendelea.

“Hatuwezi kufika mbali ikiwa hakuna usawa wa kijinsia,takwimu znaonyesha watoto wengi wanashindwa kumaliza masomo kutokana na unyanyaswaji pamoja na mimba wakiwa shuleni, lazima kila mwanajamii akemee vitendo hivi ili tufikekie maendeleo endelevu.” Alisema.

Alisema mikakati ya kufikia maendeleo endelevu yameanza ambapo sera mbalimbali zimeshatungwa ikiwemo kupinga ukatili,utoaji wa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari pamoja na uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi kwa kuwaweka karibu a taasisi za kifedha.

Kwa upande wao wawakilishi wa umoja wa mataifa walisema wapo tayari kuisaidia Tanzania katika kupambana kufikia  maendeleo endelevu huku wakiyaomba makundi maalum kuwa karibu na ofisi zao ili kutatua janga la umasikini.

Akizungumza katika kongamano hilo, Amon Manyama ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa progamu ya maendeleo endelevu, alisema katika kutekeleza ahadi za kufikia maendeleo endelevu, wanataoa kipaumbele kwa makundi maalum na kwamba wapo tayari kukaa nao meza moja kujadili changamoto zao.

Alisema kila mtu anahaki ya kupata haki za kibinadamu na hivyo kutokana na makundi hayo kusahaulika wameamua kuwapa kipaumbele ili yapate haki zao za msingi ikiwemo kuwa na maisha bora na kukua kiuchumi.

“Kutokana makundi haya yamesahaulika kwa siku nyingi, tunatoa kipaumbele kwao na tunawakaribisha katiaka ofisi zetu, tukae, tujue changamoto zinazowakabili pamoja na kuzitatua, tunataka kuhakikisha makundi maalum yanaopata haki za msingi.” Alisema Manyama.

Malengo 17 yaliyoekwa na Umoja wa Mataifa katika kufikia maendeleo endelevu hadi kufikia 2030 ni pamoja na kuondoa umasikini, kuwepo kwa usawa na kupata haki zote za kibinadamu.

No comments:

Powered by Blogger.