LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
 


TELEGRAMS:   POLISI,                                                                                                OFISI YA
TELEPHONE: 2500712                                                                         KAMANDA WA POLISI,
Fax: 2502310                                                                                            MKOA WA MWANZA,
E-mail: mwapol@yahoo.com                                                                                     S.L.P. 120,
           rpc.mwanza@tpf.go.tz                                                                                  MWANZA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 07/11/20

·       WATU WAWILI WAMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA KUANGUKIWA NA KANOPI YA JENGO LA GHOROFA MOJA WILAYANI NYAMAGANA.

Kwamba tarehe 6.11.2016 majira ya saa 11:30 katika eneo la mtaa wa Buganda kata ya Mkolani wilaya ya Nyamagana jiji na mkoa wa Mwanza, watu wawili waliojulikana kwa majina ya, 1. Twalib Nassib miaka 18, kibarua wa ujenzi na mkazi wa Buganda, na 2. Yusuph Masunga miaka 32, kibarua wa ujenzi na mkazi wa Buganda, wamefariki dunia katika ajali ya kuangukiwa na kanopi ya jengo la ghorofa moja wakati wakiendelea na shughuli za ujenzi katika nyumba hiyo.

Inadaiwa kuwa marehemu walikuwa wamepewa kibarua cha kuzibua mtaro uliopo pembeni mwa jengo hilo na mmiliki wa jengo hilo bwana Gaston David @Ikoko miaka 56, ndipo ghafla  ajali hiyo ilitokea na kupelekea wote wawili kupteza maisha.

Jeshi la polisi linamshikilia mmliki wa jengo hilo bwana Gaston David kwa mahojiano zaidi, aidha uchunguzi wa awali umebainisha chanzo cha ajali ni ujenzi wa jengo uliokuwa chini ya kiwango. 

Miili ya marehemu wote wawili imehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi wa polisi Augustino Senga anatoa rai kwa wakazi wa jiji na mkoa wa Mwaza akiwataka kuwa makini wakati huu wenye mvua nyingi, kuacha kukaa katika maeneo hatarishi ili kuweza kuepuka vifo na ajali zinazoweza kuepukika.

Imetolewa na:
ACP: Augastino Senga
Kaimu Kamanda wa polisi (M) Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.