LIVE STREAM ADS

Header Ads

UJENZI WA RELI MPYA NA YA KISASA NCHINI WAANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying IMG_20161110_100333.jpgNa James Salvatory, BMG Dar
Ujenzi wa reli mpya  ya kisasa (Standard Gauge) yenye urefu  wa kilomenta za mraba 1,219 kutoka Dar es salaam, Isaka na Mwanza imeanza kujengwa ambapo itachukua muda wa miaka mitatu kukamilika.

Akizungumza jana Jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Rahaco, Masanja Kadogosa, alisema kuwa ujenzi wamradi huo utakuwa ni wa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza itajumuisha Isaka mwanza kilometa 1219 ambapo jumla yashilingi biloni 3.694 zitatumika katika kukamilisha mradi huo.

Aidha alisema awamu ya pili itakuwa Tabora -uvinza ,kigoma km411 ambapo zaidi ya bilioni 6.7145  isaka -rusumo km371 ,keza -ruvubu (km36 bilioni 4,926 wakati uvinza hadi kalema hadi msogati km203 ambapo bilioni 0.538 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo

Alibainisha kwamba zoezi la utekelezaji wa miradi hiyo utajumuisha hatua mbalimbali ikiwemo usanifu hadi hatua za kumpata mkandarasi wa ujenzi wa miradi hiyo ambapo miradi hiyo ininataraji wa kukamilika baada ya miaka mitatu ambapo awamu ya kwanza ya ujenzi huo itanza Dar es salam hadi Mwanza 

No comments:

Powered by Blogger.