LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIFO VYA AKINA MAMA NA WATOTO NCHINI BADO NI CHANGAMOTO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Displaying IMG_20161111_125001.jpg
Mkurugenzi mkuu wa shirika la Thamini Uhai  Dr.nguke Mwakatundu, akizungumza kwenye uzinduzi wa shirika hilo.

Na James Salvatory, BMG Dar
Vifo vya akina mama na mtoto bado ni tatizo nchini kutokana na tafiti za mashirika ya Kimataifa kuonesha kwamba Tanzania inashika nafasi ya nne Afrika na nafasi ya sita duniani kwa vifo vya akina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa shirika la Thamini Uhai jijini Dar es salaam, Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Dkt.Nguke Mwakatundu, alisema kuwa katika kuthamini uhai wa binadamu wamesaidia kuboresha vituo vya Afya vijijini na kuwasaidia kinamama wanaojifungua kuepuka hatari mbalimbali ambazo zinaweza kuwasababisha vifo

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa afya ya mama na mtoto toka Wizara ya Afya aliitaka jamii ishiriki katika kumsaidia mama kujifungua salama huku vituo vya afya vikitakiwa kuwa na wataalamu wakutosha kwa wakati pindi mama anapofikishwa apatiwe huduma kwa haraka kwani 85% ya kinamama wanauwezo wa kujifungua salama endapo wakipatiwa huduma muhimu.

Aidha aliongeza kuwa serekali inamipango mingi ya kukabiliana na tatizo la vifo kwa mama na mtoto ila utendaji bado ni mdogo uchache wa watoa huduma na vifaa tiba hivyo ni vyema iwekwe mikakati ya dhati ya kukabiliana na tatizo hilo.

No comments:

Powered by Blogger.