LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAWEKEZAJI KUTOKA UCHINA WABANWA NA SERIKALI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Katika kuhakikisha serikali inapata mapato yake ipasavyo kupitia kodi, wawekezaji kutoka nchini china wamepaswa kujisajili katika kituo cha uwekezaji nchini (TIC) pamoja Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya Mapato nchini, Richard Kayombo, katika ufunguzi wa semina ya kumi na tano ya miongozo na sheria za ulipaji kodi nchini ambapo amesema kuwa ili kuweza kukuza sekta yaviwanda nchini china ni mdau mkubwa katika suala zima la uwekezaji hivyo ni vyema wafanyabishara nawawekezaji katika nchi hiyo kuweza kuzifahamu taratibu na kanuni za ukwekezaji .

Aidha Kayombo alisema anataka China iweze kuleta viwanda ili kuwawezesha vijana wetu waweze kupata ajira lakini kama dira ya serikali ya awamu ya tano imelenga ukusanyaji wakodi mbalimbali ikiwemo kodi za mapato ,lakini pia tunataka wadau wetu hasa wasekta ya uwekezaji kuweza kuzifahamu sheria za uwekezaji na ulipaji wa kodi ilikuweza kuhahakikisha Tanzania inafikia katika dira yauchumi wa viwanda.

Alisema kuwa kumekuwa changangamoto mbalimbali ambazo zimekuwa ni kikwazo katika sekta ya uwekezaji nchini ikiwemo Baadhi ya wawekezaji kutofahamu sheria na kanuni za uwekezaji nchini jambo linalochangia sekta hiyo kurudishwa nyuma .

Alibainisha ni wakati mahususi kwa viwanda vilivyofungiwa china kuja kuwekeza hapa nchini kwani viweza kuchochea uchumi waviwanda nakuiwezesha Tanzania inafikia katika uchumi wakati kama ilivyo nchi ya chinil

Kaimu Mkurugezi wa Viwanda na Biashara cliford Tandari amewataka wawekezaji wakutoka china kuweza kujenga viwanda ilikuweza kukuza mazingira mazuri yakibiashara ili tanzania na china waweze kunufanika na uwekezaji huo.

No comments:

Powered by Blogger.