LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI ATAKA BODI MPYA YA SHIRIKA LA RELI NCHINI KUZINGATIA UADILIFU KAZINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying IMG_20161116_115115.jpgNa James Salvatory, BMG Dar
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameitaka bodi mpya  ya shirika la Reli nchini (TRL) kuwa uadilifu ili kulikuza shirika hilo.

Akizungumza jana kwenye uzinduzi wa bodi ya shirika hilo jijini Dar es salaam, Profesa Makame Mbarawa, aliitaka bodi ya shirika hilo kuwa na ubunifu na kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuweza kukuza mapato ya shirika hilo ambalo limekuwa ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania.

Aidha Mbarawa alisema kuwa katika kipindi cha bajeti ya mwaka huu serikali ya awamu yatano imetenga bajeti ya shilingi trioni moja ili kuweza kuboresha miundombinu ya reli nchini ambapo reli mpya itajengwa katika  Mikoa ya Morogoro ,Tabora  hadi mwanza kwa kiwango cha standard gauge.

''Tayari Makandarasi arobaini wameshajipanga juu ya usanifu na ujenzi huu wa reli sambamba na ujenzi wa treni ya  pia tutajenga karakana ya kisasa hii ndio TRL ya Mbarawa ''alisema Mbarawa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya shirika la TRL John Wanyanja, alimshukukuru waziri makame mbarawa kuweza kuiteua na kuweza kuahidi kuwa kutekeleza maagizo ya liyotolewa na waziri huyo.

No comments:

Powered by Blogger.