LIVE STREAM ADS

Header Ads

ALIBHAI AZINDUA KAMPENI ZAKE JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Uwanja wa Nyamagana
Judith Ferdinand, Mwanza
Mgombea Ujumbe Mkutano Mkuu Chama cha Soka nchini TFF katika uchaguzi mkuu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mwanza unaotarajia kufanyika mapema januari saba mwakani, Aleem Alibhai amezindua kampeni zake.

Alibhai alizindua kampeni hizo jana jijini Mwanza, na kutaja vipaumbele vyake ambavyo atasimamia na kutekeleza kwa vitendo,endapo atapatiwa ridhaa kwa kuchaguliwa katika uchaguzi huo.

Alisema, moja ya mambo atakayosimamia ni pamoja na kuhakikisha mwakani mkoa unatoa timu tatu zitakazo shiriki ligi kuu (VPL), kwa kusaidia  timu ya Mbao kuendelea kufanya vizuri, Toto haishuki daraja na Alliance inapanda daraja,kwa kushirikiana na kamati tendaji na wadau mbalimbali.

Pia alisema, atashirikiana na kamati tendaji pamoja na vyama vyote vinavyohusiana na mpira wa miguu kama Chama cha Waamuzi na Makocha mkoa,kuhakikisha wanapunguza kasoro zilizopo,ili kuwa na  bora  timu bora zitakazoshiriki ligi zote na kufikia mwaka 2020,mkoa uweze kutoa timu tano zinazoshiriki ligi kuu.

Aidha alisema, hatahakikisha kuna kuwa na umoja kikanda na mkoa,ili kuendeleza michezo na kutoa timu nyingi zitakazo kuwa zinashiriki ligi mbalimbali.

Vilevile alisema, atasaidia kuwepo kwa utoaji wa tuzo za MZFA,kwa ajili ya wadau wanaojitolea na kuhakikisha mchezo wa mpira wa unasonga mbele,ili kuwahamasisha zaidi na kutambua mchango wao.

Kadhalika alisema,ili kuendeleza mchezo kwa watoto ataziunga mkono academy zote zilizopo na zitakazo anzishwa pamoja na kushawishi vilabu vyote mpira wa miguu kuanzia ngazi zote,kuruhusu watoto kuingia bure.

Hata hivyo alisema, endapo atapatiwa nafasi hiyo, atajitahidi  kuleta mafunzo/ kozi nyingi kwa makocha ili kuendeleza mpira katika Mkoa.

Pia aliwai kushika uongozi wa nafasi mbalimbali katika timu ya Pamba,na yupo tayari kisaikolojia kwani anauzoefu wa kutosha.

Licha ya kuwa na vigezi, ndiye aliyeandikia pendekezo kwa TFF june mwaka 2014 la kuanzishwa kwa ligi daraja la pili na mwezi Oktoba mwaka huo ikatangazwa rasmi kuanza.

No comments:

Powered by Blogger.