LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHUO CHA KODI NCHINI CHAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Chuo cha Kodi ambacho ni sehemu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jana kimewatunuku vyeti  wanafunzi  558 katika mahafali ya tisa ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kupitia chuo hicho, Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutunuku  Astashahada ya Uzamili  katika uongozi wa forodha ya Afrika  Mashariki, jumla ya wahitimu 77 wametumukiwa PGCCA, wote kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mkuu wa chuo hicho, Profesa Isaya Jairo, alisema changamoto zinazowakabili  wanafunzi wengi wa chuo hicho ni pamoja na kushindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya kukosa ada na fursa ya kupata  mikopo, vitendea kazi na miundombinu.

Aidha aliwapongeza wahitimu wa chuo hicho walioweza kumaliza masomo yao na kuwahimiza kuwa mabalozi wazuri katika jamii kwa kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa ulipaji wa kodi.

No comments:

Powered by Blogger.