LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKAMU MKUU CHUO CHA SAUT AOMBA WANAFUNZI WANAOTOKA FAMILIA MASKINI WASAIDIWE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Makamu Mkuu wa Chuo  cha Mtakatifu Augostine Tanzania  (SAUT), Dk. Thadeus Mkamwa
Judith Ferdinand, Mwanza
Serikali yashauriwa kutafuta njia mbadala kwa ajili ya kunusuru vijana waliopo vyuoni hususani kutoka familia masikini,  kwani wanategemea pesa za mikopo kwa kila  jambo.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Makamu Mkuu wa Chuo  cha Mtakatifu Augostine Tanzania  (SAUT), Dk. Thadeus Mkamwa katika mahafali ya 18 ya chuo hicho, ambapo wahitimu 2652 walitunikiwa shahada, stashahada na astashahada mbalimbali huku 664 wakishindwa kuhitimu kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kifedha na kitaaluma.

Alisema ingekuwa ni jambo jema kama mikopo wangepewa wanafunzi wanaotoka katika familia zinazoweza kulipa kwani hao wanakopesheka huku wanaotoka katika familia maskini wapewe misaada au udhamini lakini wawe wametimiza vigezo huwezi  kuwapa mikopo watu masikini ambao hawawezi hata kulipa ada kidogo maskini hawezi kukopesheka iwe  mtu au nchi.

Hata hivyo alisema, serikali inatakiwa kushirikiana na taasisi zake na asasi zisizo za serikali kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu, ili kwa pamoja waweze kuboresha na kukuza elimu nchini itakayoangalia mfumo mzima wa elimu na siyo kwenye kusahihisha mitihani au kupanga madaraja tu.

Pia alisema,kuhusu fikra na maneno yanayoenezwa   kutoka vyombo vya serkali ,wizara na bodi mbalimbali kuwa vyuo vikuu Tanzania ni vingi  na vinatumia pesa ya serkali kujijenga,umefika muda wa kuvifunga au kupinguzwa pasipo kujua vyuo vikuu ni kwa faida ya watanzania na hakuna uhusiano wowote kati ya wingi na sifa za vyuo kukidhi haja na viwango vinavyotakiwa.

" Tutakapo vifunga vyuo vikuu bila sababu ya msingi, tujiandae kujenga magereza mengi pia, " alisema Mkamwa.

Naye mgeni rasmi Askofu mkuu Jimbo Kuu la Mwanza Yuda Ruwa’ichi ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Chuo ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania na Askofu wa Jimbo la Iringa Tarcisius Ngalalekumtwa alisema, ikumbukwe kuwa vyuo vikuu ni chachu ya maendeleo ya taifa kupita kazi zake za kufundisha, kufanya utafiti na huduma kwa jamii.

Alisema amefarijika kusikia baadhi ya mafanikia yaliyoyapata SAUT pamoja na vyuo vyake shirikishi kwa mwaka wa masomo 2015/2016 wamefanikiwa kutoa wahitimu 3000 katika fani mbalimbali kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada ya uzamili na kuongeza idadi ya wataalamu katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya taifa letu.

Hivyo aliwataka wahitimu kuwa na nidhamu, uzalendo na maadili kwani taifa ndilo linawahitaji kwa wingi wasomi wa namna hiyo ndio watakao changia kuijenga nchi katika misingi endelevu ya utu, upendo na kutanguliza maslahi ya wengi hususani wanyonge na maskini.

Kwa upande wao wahitimu wa kozi mbalimbali Bright Muchungwi na Leah Urasa wakizungumza kwa niaba ya wenzao walisema wanamshukuru mungu kwa hatua waliofikia na wamejengewa mazingira na chuo ya kufanya kazi sehemu zozote na kupambana ili kufikia malengo na kuepuka kufuata mkumbo.

Aidha walisema elimu waliopata wanaingia mitaani ili kujitafutia ajira kwani sio busara kusubili serikali kuwatafutia ajira kuhusu kulipa mkopo walisema hawana ajira hivyo pesa walizokopeshwa hawawezi kulipa  mpaka pale watakapopata ajira lakini ingekuwa ni jambo jema sana serikali ingetuangalia kwa jicho la tatu kukapata misaada kuliko mikopo.
Tazama Picha HAPA

No comments:

Powered by Blogger.