LIVE STREAM ADS

Header Ads

MCHUNGAJI SALAGE WA PENTEKOSTE KAWEKAMO JIJINI MWANZA ALIA NA SUALA LA AMANI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Waamini wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini wameombwa kutunza amani iliyopo  ili kuweza kufanya mambo kwa  utulivu, hivyo kutasaidia  kuleta maendeleo na kukuza uchumi.

Ushauri huo ulitolewa jana na Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste lililopo Kawekamo B wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Emmanuela Salage.

Alisema, kwa  kudumisha amani na upendo ni vema waumini wakamtanguliza Mungu katika  kazi zao  ili kuweza kuepuka kufanya vitendo viovu.

Pia  alisema,  ni vema  wananchi wakawa na utaratibu wa kufichua watu  ambao wanafanya vitendo vya uhalifu  katika maeneo yao,  ili waweze kuchukuliwa hatua kali  za kisheria kwani kuvunja amani siyo jambo jema,  kunasababisha jamii kushindwa kufanya shughuli  za kuwapatia  kipato. 

“Tunatakiwa kujiandaa wakati wote kwa kufanya mambo mema  ambayo yanayompendeza muumba   wetukwani hakuna ajuaye siku ya kifo sambamba na  kutunza  amani ya nchi hii iliyotafutwa kwa kipindi kirefu,”alisema Salage.

No comments:

Powered by Blogger.