LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA WATAKIWA KUUINUA MCHEZO WA MPIRA WA KIKAPU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Wadau mbalimbali mkoani Mwanza, wamehimizwa kusaidia kutatua changamoto zinazoukabili mchezo wa mpira wa Kikapu, ikiwemo viwanja ili  kuinua vipaji na kuendeleza mchezo huo.

Wito huo ulitolewa jana na Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Angelina Mabula, wakati akifungua bonaza la siku mbili la mchezo wa mpira wa kikapu kwa watoto chini ya umri wa miaka 13 na 15, katika uwanja wa Kiloleli wilaya Ilemela mkoani hapa,yaliyoandaliwa na Mratibu wa mchezo wa Mpira wa Kikapu Mkoa wa Mwanza Kizito Bahati.

Mabula alisema, mchezo wa mpira wa kikapu ndio umeanza, ataendelea kuunga mkono juhudi hizo, ili kukuza na kuendeleza mchezo huo kama mkoa wa Dar es salaam,hivyo wadau wajitokeze kusaidia.

Kwa upande wake Mratibu wa mchezo huo, Kizito Bahati, alisema, bonanza ilo limeshirikisha timu kutoka mkoa wa Dar es saalam, ikiwa ni muendelezo wa mafunzo ya mchezo wa mpira wa kikapu kwa  watoto katika mkoa wa Mwanza.

Pia alizipongeza timu za Mwanza kwa kujitahidi kucheza licha ya kutoshinda mchezo wowote,kwani ndio mara yao ya kwanza kucheza ligi tangu kuanzishwa kwa mafunzo hayo.

Naye Kocha wa  timu ya  Kiloleli Youth, Khamis Kaphy, alisema, changamoto inayokabili mchezo huo ni uwepo wa watoto wengi sehemu moja na uhaba wa viwanja kwa ajili ya mchezo huo.

Hata hivyo mmoja wa wachezaji kutoka Nyasaka, Juma Yusuph, alisema anapenda mchezo wa mpira wa kikapu kwa vile unazingatia sheria,ila ukosefu wa viwanja unapelekea mchezo huo kuto endelea,hivyo anaomba wadau wasaidie mchezo huo,ili kukuza vipaji na kuwa kama mpira wa miguu.

Aidha kocha wa timu ya Rising Stars kutoka Dar es saalam, Issa Hudadadi, alisema ili kuendeleza mchezo huo lazima uanzie ngazi ya shule pia wazazi wawaruhusu watoto wao kucheza huku viwanja viwe sehemu ambayo watoto wataweza kufika kwa urahisi.

No comments:

Powered by Blogger.