LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YA QATAR YAIPIGA JEKI WIZARA YA AFYA NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying IMG_20161207_150333.jpgNa James Salvatory BMG Dar
Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  jana amepokea  jumla ya Magari 10 ya kubebea Wagonjwa (Ambulance) kutoka Serikali ya Qatar.

Mwalimu aliishukuru Serikali ya Qatar kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na kuahidi kuyatunza magari hayo na kwenda kwenye maeneo yote yaliyokusudiwa na kipaumbele zaidi ni pamoja  kwenda kusaidia wanawake wajawazito na watoto huku magari hayo yakilengwa kwenda katika maeneo yenye uangalizi maalum ikiwemo yale yenye kutokea ajali za mara kwa mara.

Alisema kuwa magari  hayo yanatarajiwa kwenda katika maeneo mbalimbali ikiwemo mkoa wa Morogoro, Tanga, Tabora, Kagera pamoja na maeneo ya mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo wameona kuna umuhimu zaidi ,Pia kwa Dar es Salaam magari hayo mengine yatapelekwa Wilaya ya Kigamboni na lingine katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo yatasaidia kusafirisha wagonjwa kutoka Hospitalini hapo kwenda uwanja wa ndege kwa ajili ya safari za matibabu.

Kwa upande wake balozi wa Qatar, Mh. Abdulla Al Suwaid aliyewakilisha serikali ya Qatar alibainisha kuwa, Serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimalisha mambo mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya.

No comments:

Powered by Blogger.