LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAASISI YA OJADACT YASIKITISHWA NA KUKAMATWA KWA BAADHI YA WANAHABARI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo
Chama cha Waandishi wa habari wanaopiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Ojadact, kimelaani suala la baadhi ya wanahabari kukamatwa wakitimiza majukumu yao kutokana na amri za baadhi ya viongozi wa serikali.

Mwenyekiti wa chama hicho, Edwin Soko, ametoa kauli hiyo jijini Mwanza wakati akizungumza na Lake Fm kuhusiana na hofu inayoweza kuwakumba wanahabari kutokana na kamata kamata hiyo.

"Kitu chochote duniani ni maridhiano, kuwa na sheria kali haisaidii. Hawa viongozi wakae na wanahabari wajenge maridhiano kwa sababu taaluma ya habari ina misingi na kanuni zake hivyo isifikie tu siku mkuu wa wilaya au mkoa anasema hii habari ni ya uchochezi, je nani nani anapima uchochezi". Amesisitiza Soko.

Baadhi ya waandishi wa habari jijini mwanza wamesema ushirikiano zaidi miongoni mwao na viongozi wa serikali unahitajika badala ya kuwekewa mazingira magumu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Majuzi mwanahabari wa ITV mkoani Arusha, Khalfan Liundi alikamatwa kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Arumeru kwa kumtuhumu kuripoti habari ya uchochezi ambayo ni wananchi wa eneo la Usa-River kulalamikia kukatiwa maji kwa takribani wiki nzima.

No comments:

Powered by Blogger.