LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAHADHARI YA POLISI MKOANI MWANZA KWENYE SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2017.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi
#LakeFmHabari

Na George Binagi-GB Pazzo
Jeshi la polisi limewataka wananchi kusherehekea kwa amani Sikukuu ya Christmass hapo kesho Disemba 25, na mwaka mpya 2017 ambapo limesema limejipanga vyema kupambana na aina zote za vitendo vya uvunjifu wa amani

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, amesema jeshi hilo limejipanga kuhakikisha linaimarisha ulinzi katika maeneo yote ikiwemo kwenye nyumba za ibada pamoja na maeneo ya starehe

Kamanda Msangi amesema jeshi hilo limepiga marufuku uwepo wa disko toto kwenye kumbi za starehe na kwamba wenye nia ya kuandaa michezo ya watoto waandalie kwenye maeneo ya wazi huku pia likizuia suala la vilipuzi mitaani kwa watu wasio na vibali.


Aidha kamanda Msangi amewataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo ili kuimarisha ulinzi katika maeneo yao ambapo amewasihi wananchi kutoondoka wote katika makazi yao bila kuacha mtu yeyote.

No comments:

Powered by Blogger.