WAUMI WA DINI YA KIISLAMU NCHINI WASHEREHEKEA SIKUKUU YA MAULID.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Waumini wa dini ya Kiislamu nchini leo wanaungana na
wenzao kote ulimwenguni kusherehekea Sikukuu ya Maulid ambayo ni kumbukumbu ya
kuzaliwa kiongozi wao Mtume Muhammad.

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubery amesema dua
ya Maulid imefanyika jana usiku na baraza la Maulid limefanyika asubuhi hii katika
tarafa ya Shelui mkoani Singida ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa
mgeni rasmi.
Mufti Zubery
amewataka watanzania hasa wenye uwezo kuwahurumia wasio na uwezo ambapo amesema
mtume mohammad alifundisha kuwa dini imekuja kutunza upendo na Amani.
#LakeFmHabari
No comments: