LIVE STREAM ADS

Header Ads

YALIYOFANYIKA WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA 2016.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

maandamano
Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 kuelimisha jamii kuzuia ukatili wa kijinsia. WiLDAF inashirikiana na mtandao wa mashirika yanayopinga ukatili wa kijinsia (MKUKI), wadau wa maendeleo na mashirika mengine kuadhimisha kampeni hizi kitaifa.

Yafuatayo ni matukio mbalimbali ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili kama yalivyofanyika sehemu mbalimbali nchini Tanzania chini ya kauli mbiu: Funguka! Pinga ukatili wa kijinsia. Elimu salama kwa wote.

Maandamano ya amani kupinga ukatili wa kijinsia Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa jiji la Dar es salaam ulianza kwa maandamano ya amani ambapo maelfu walishiriki maandamano hayo kutoka Biafra hadi Millenium towers jijini Dar es salaam. Maandamano hayo yalifanyika tarehe 25 Novemba 2016. 
maandamano2    
Waziri Ummy Mwalimu mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alikua mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho hayo yaliyofanyika tarehe 25 Novemba 2016, jijini Dar es salaam. 

 Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Ummy alisema serikali ya awamu ya tano imefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba watoto wanapata elimu salama bila aina yoyote ya ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa elimu bora bila malipo. 

"Lengo kuu la elimu bila malipo ni kuhakikisha kuwa watoto wetu hususan wa kike wanapata fursa ya kwenda shule kusoma na kufikia ndoto zao katika maisha."

Aidha alitoa wito kwa wadau na serikali kwa ujumla kutumia nafasi zao kupinga vitendo vyote vya udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za binadamu vilevile kwa jamii kuwa na malezi bora na kuzingatia maadili kwa watoto na vijana wetu.
 
Mama Anne Makinda mgeni rasmi katika kongamano la kitaifa la Haki za Wanawake. 

 Aliyekuwa spika wa Bunge la Tanzania mama Anne Makinda alikuwa mgeni rasmi katika kongamano la kwanza la kitaifa la Haki za wanawake lililofanyika ukumbi wa Millenium Towers jijini Dar es salaam tarehe 28 Novemba 2016.

Kongamano hilo lililoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la LSF lilikuwa na lengo la kujadili namna mbalimbali za kuwawezesha wanawake kisheria na kiuchumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Jamii imeaswa kuhusika kikamilifu katika mapambano ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuhakikisha watoto wanapata elimu bora na salama. Kongamano hilo lilipambwa na kauli mbiu isemayo; Jitambue! Jiamini, Simamia Haki yako.

Wageni mbalimbali wanaharakati wa Haki za binadamu walihudhuria kongamano hilo la aina yake wakiwemo Dr. Helen Kijo Bisimba, Mary Rusimbi, Edda Sanga na Dr. Judith Odunga.
mama-makinda Mkuu wa Wilaya ya Rungwe azindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Challya Julius alizindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika wilaya yake na kuahidi kusimamia katika kutokomeza ukatili wa kijinsia wilayani humo. 

Uzinduzi huo ulifanyika 29 Novemba 2016. Uzinduzi huo ulienda sambamba na kutoa msaada wa kisheria kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia uliotolewa na wasaidizi wa kisheria (Paralegals) wa wilaya ya Rungwe wakishirikiana na shirika la WiLDAF Tanzania.
mhe-challya Jukwaa la Wanafunzi wakati wa maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wa kidato cha 1, 3, 5 na 6 kutoka shule za sekondari za Benjamin Mkapa, Jangwani, Tandika, Turiani na Temeke walihudhuria jukwaa lilioandaliwa kwa ajili ya wanafunzi ili wapate fursa ya kutoa maoni juu ya mambo mbalimbali yanayowakabili mashuleni. Jukwaa hilo lilifanyika 30 Novemba 2016 katika ukumbi wa Millenium Towers jijini Dar es salaam. jukwaa-la-wanafunzi Jukwaa hilo liliandaliwa na shirika la WiLDAF Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Funguka! Pinga Ukatili wa Kijinsia. Elimu Salama kwa wote. jukwaa-la-wanafunzi2 Siku ya UKIMWI Duniani
Januari mosi kila mwaka hutumika kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani. Maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa asilimia kubwa yanatokana na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake vinavyopelekea maambukizi ya VVU kama vile ubakaji, mila mbalimbali ambazo zimepitwa na wakati kwa mfano: - - Ndoa za utotoni ambapo mtoto wa kike hulazimishwa kuolewa na mtu mzima ambaye pengine ana maambukizi ya VVU.

- Mume kumlazimisha mke kufanya tendo la ndoa iwapo mume ameathirika bila kutumia kinga. - Mjane kulazimishwa kufanya ngono na mzee anayetakasa wajane. - Na wajane kulazimishwa kurithiwa na ndugu wa mume wake bila kujali afya ya wote wawili. Jamii inapaswa kuacha na kukemea mila zilizopitwa na wakati ili kupunguza maambukizi ya UKIMWI.
  siku-ya-ukimwi Mdahalo wa wadau wa maendeleo kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. 
 Wadau wa maendeleo kutoka mashirika, serikali na taasisi mbalimbali walikutana pamoja ili kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusiana na ukatili wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Mdahalo huo ulifanyika Desemba 1, 2016.
wadau-wa-maendeleo-1
Hizi ni baadhi ya nukuu kutoka katika mdahalo huo;
"Ukatili wa kijinsia huanzia nyumbani, shuleni na kwenye jamii. Jamii ipatiwe elimu ya kutokomeza ukatili." "Wazazi wawe na ukaribu na watoto katika malezi na kujua mienendo ya watoto wao." "Hakuna mtoto anayezaliwa akiwa mtukutu ila inatokana na malezi ya nyumbani na muda mwingine kupeleka hivyo vitu shuleni na hata kuwafanyia watoto wengine vitendo vya kikatili." "Ukatili wa watoto unafanywa na ndugu wa karibu wa nyumbani anaweza akawa mjomba, dada wa nyumbani." "Fimbo sio solution (suluhu) ya kumrekebisha mtoto, itafutwe njia mbadala ya kumuadhibu mtoto."
wadau-wa-maendeleo-2
  Vibanda vya Filamu Katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, shirika la TGNP Mtandao liliandaa vibanda vya filamu ili kujenga uelewa kwa jamii na kuibua mjadala juu ya vitendo mbalimbali vya ukatili.
vibanda-vya-filamu
Wawakilishi wa Bodaboda wapata mafunzo ya ukatili wa kijinsia, waandamana kupinga ukatili. Wawakilishi wa madereva wa bodaboda kutoka Wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke mkoa wa Dar es salaam walipata mafunzo juu ya ukatili wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Madereva bodaboda wanahusika katika kubeba abiria mbalimbali wakiwemo wanafunzi hivyo ni muhimu kuwapatia elimu hii ili waweze kutambua madhara ya ukatili na kusaidia kuilinda jamii dhidi ya vitendo vya ukatili.
Aidha madereva hao waliungana na shirika la WiLDAF kuandamana kama ishara ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
bodaboda
Kauli mbiu ya maadhimisho ni FUNGUKA! PINGA UKATILI WA KIJINSIA. ELIMU SALAMA KWA WOTE. 
 Kauli mbiu hii inakusudia kuhamasisha jamii na taifa kwa ujumla kuangalia ni kwa kiasi gani changamoto zilizopo katika miundombinu, mifumo ya kibaguzi na kukosekana kwa usawa wa kijinsia, sio tu kunachochea ukatili wa kijinsia, bali pia kunakwamisha juhudi za serikali, asasi za kiraia na wadau mbalimbali katika kuboresha elimu na hivyo kusaidia watanzania kujikwamua katika wimbi la ujinga na umaskini. #UkatiliSasaBasi  
Blog za Mikoani

No comments:

Powered by Blogger.