LIVE STREAM ADS

Header Ads

ZAIDI YA ASILIMIA 50 YA WATANZANIA HAWAJAWAHI KUIONA KAIBA INAYOTUMIKA SASA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Displaying IMG_20161208_110046.jpgNa James Salvatory, BMG Dar
Imeelezwa kuwa asilimia 50 ya watanzania hawajawahi kuiona katiba ya sasa  huku katika watanzania 10 Ambao waliwahi kuiona katiba hiyo, ni watu watatu tu ambao waliisoma

Akizungumza jana katika semina ya siku moja ya utafiti na uelewa wa katiba kwa watanzania iliyolenga juu ya uwelewa wa katiba kwa wananchi, Mkurugenzi wa  kitaifa wa kampuni ya  Sung consultant's, Haron Sungusia, alisema kuwa walifanya utafiti kwa Mikoa 20 kwa lengo la kujua uelewa  wa katiba ya mwaka 1977 na  katiba ya zanzibar ya 1984 na rasimu ya Jaji Mstaafu, Joseph Warioba na katiba mpya  ambapo waligundua asilimia 50 ya watanzania hawajawahi kuiona katiba ya sasa  huku katika watanzania 10 Ambao waliwahi kuiona katiba ya sasa ni watatu  tu ambao waliisoma

Aidha  Sungusia alisema kuwa baada ya uchunguzi huo walipendekeza  mitaala ya elimu iboreshwe kwa kuweka somo la katiba katika shule  na mikoa ambayo inaongoza kuwa nyuma kwa masuala ya kikatiba kiwekea mikazo katika   mpango wa taasisi mbalimbali klza kushughulikia katiba mbalimbali

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria, Harison Mwakiyembe, alisema kutokana na taarifa hiyo kuonyesha mapungufu hayo, serikali itachukua hatua za makusudi kuhakikisha katiba ya sasa au itakayokuja inawafikia wananchi, kwa kshirikiana na vyombo vya habari kwa lengo la angalau kwa kila siku kuweka vipengele viwili au vitatu ili wananchi waweze kuielewa

Utafiti wa uelewa wa katiba kwa watanzania iliyolenga  juu ya uwelewa wa katiba kwa wananchi ulihusisha mikoa 20 ya Tanzania  Bara (wilaya 45) huku kwa upande wa Tanzania Zanzibar ukihusiashwa  wilaya 10 ambapo jumla ya wilaya 55 kwa Tanzania nzima zilihusishwa.

Displaying IMG_20161208_112020.jpg

No comments:

Powered by Blogger.