LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA WILAYA YA ILALA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA CHINA.

Na James Salvatory, BMG Dar Mkuu wa wilaya ya Ilala mkoani Dar es salaam, Sophia Mjema, jana amekutana na ugeni kutoka nchini China (Jimbo la Jiang Su, Manispaa ya xuzhou) na kukubalina mambo mbalimbali yenye tija kwa maendeleo ya wilaya hiyo.

Mjema alisema ugeni huo unatija kwa wilaya yake kwani miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni namna ya kuipendezesha wilaya ya Ilala ili ifanane na maeneo mbalimbali ya nchini China kwa kuzingatia usafi wa maeneo husika, ujuzi wa kiusalamaikiwemo  vifaa vya kisasa ambacho China huvitumia kupambana na uhalihu.
Aidha alisema China itasaidia  kuchochea maendeeonchini hususani kwenye sekta ya viwanda aliyokuwa anainadi Rais John Magufuli kipindi cha kampeni za urais, na kusisitiza kuwa yapo maeneo mbalimbali kwa ajili ya uwekezaji.

Katika hatua nyingine Mjema alieleza kwamba China ilikuwa sawa na Tanzania miaka 20 iliyopita lakini nidhamu na bidii ya kufanyakazi ndiyo imesababisha taifa hilo kufika kupiga hatua kimaendeleo hivyo Watanzania waige kuiga mfano huo ili kufikia malengo ya mapinduzi ya kiuchumi.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka  China, Makamu Mwenyekiti wa kamati ya jimbo Jimbo la Jiang Su , Zhang Aijun, alisema China kupitia jimbo hilo iko tayari kushirikiana na wilaya ya Ilala ikiwemo kufanya uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya pande zote mbili.

No comments:

Powered by Blogger.