CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI GEITA CHALAANI WANAHABARI KUSHAMBULIWA NA POLISI.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mwenyekiti wa chama cha waanishi wa habari(GPC) mkoani Geita Daniel Limbe akitoa tamko na kulaani vikali tukio walilofanyiwa waandishi wa habari juzi baada ya msafara wa Edward Lowassa kuzuiliwa na polisi mkoani humo.
Waandishi wa habari mkoani Geita wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mwenyekiti wa GPC
Viongozi wa GPC wakiwa kwenye kikao na waandishi wa habari, kulia ni Victor Bariety ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho na kushoto ni katibu wa GPC Salum Maige.
Chama cha waandishi wa habari Mkoani Geita(GPC) kimelaani vikali kitendo cha kushambuliwa kwa waandishi habari na jeshi la polisi wakati wakiwa katika majukumu yao ya kikazi.
MadukaOnline
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ,mwenyekiti wa chama hicho Mkoani humo, Daniel Limbe,amesema kuwa swala lililofanyika kwa kushambuliwa kwa waandishi wa habari ni mwendelezo wa jeshi hilo kuminya uhuru wa habari kwa watanzania ambao walipenda kujua ni kipi ambacho kilijiri siku ya juzi.
“Kama chama cha waandishi Mkoani Geita, tumesikitishwa sana na kitendo cha jeshi polisi kuwavamia waandishi na kuwapiga sisi kama chama tumeona hatuwezi kukaa kimya swala hili tunalilaani vikali kwani ni mwendelezo wa uonevu kwa waandishi wa habari hapa nchini kupitia kwa jeshi la polisi”Alisema Limbe
Hata hivyo Limbe amemtaka Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba kujitokeza hadharani na kutoa tamko juu ya tukio lililofanywa na askali ambao wamehusika na kitendo cha kuwapiga waandishi wa habari .
“Sisi kama chama cha waandishi wa habari mkoa wa Geita tunamwomba sasa Waziri wa Mambo ya ndani , Mh Mwigulu Nchemba kujitokeza hadharani na kutoa tamko dhidi ya jeshi la Polisi kutokana na unyanyasaji wanaofanya kwa wanahabari na vyombo vya habari kimsingi tunaomba asimame na kuwaeleza wa watanzania kuhusiana na tukio la jana kama vitendo vilivyo fanywa na jeshi la Polisi kama ni yake au maagizo ya mkuu wa polisi wa mkoani Geita ama ni ukiukwaji wa taratibu za kiutumishi wa vijana wa jeshi la polisi”Alisisitiza Limbe
Aidha baadhi ya wananchi Mkoani humo wamelaani kitendo walichofanyiwa waandishi wa habari kuwa swala hilo ni ukiukwaji wa sheria za nchi na kutokutoa uhuru vyombo vya habari kuripoti vitu ambavyo vinakuwa vimejitokeza.
Hali hiyo imekuja baada ya juzi kutokea kwa tukio hilo wakati waandishi wa habari wa storm fm na channel ten walipokuwa wakifatilia taarifa ya kukamatwa kwa waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne na mjumbe wa kamati kuu wa Taifa chadema,Edward Lowasa kukamatwa akiwa anatokea Mkoani Kagera wakati alipokuwa akisalimiana na wananchi kwenye eneo la stend ya zamani.
No comments: