LIVE STREAM ADS

Header Ads

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KUTOA VIPIMO VYA LISHE BURE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, Dar
Hospitali ya taifa ya Muhimbili imeanza kupima hali ya lishe kwa watu wote wanaofika katika hospitali hiyo kwa lengo la kupunguza magojwa yasiyo ya kuambuzikiza.

Akizungumza jana na wandishi wa habari wakati wa kutoa vipimo hivyo, Mtaalamu wa lishe kutoka hospitali hiyo, Mariamu Nyamwa, alisema watu wengi nchini hawazingatii ulaji bora hatua ambayo huwasababishia magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo kisukari, figo, moyo na saratani.

Nyamwa alisema kuwa kwa wale ambao watabainika kuwa na hali kubwa ya lishe kuliko kawaida watapangiwa siku za kuonana na madaktari kwa ajili ya ushauri na matibabu na kwa wale ambao watakuwa na lishe duni yaani  uwiani wa uzito na urefu hauko sahihi nao watasaidiwa.

Aisha Mbwana  ambaye ni mmoja wa watu waliopata vipimo hivyo vya lishe aliwaomba wananchi wengine kujitokeza kupata huduma hiyo kwani haina malipo na ni nzuri kwa afya

Vipimo hivi vya kupima  lishe  vimeanza leo na vinategemewa kuwepo hospitali ya taifa muhimbili kwa wiki nzima.

No comments:

Powered by Blogger.