LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI ZA MAWASILIANO YA SIMU NCHINI ZAANZA KUTII AGIZO LA SERIKALI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
102.5 Lake Fm Mwanza Studios.

Na mdau, BMG Dar
Kufuatia agizo la Serikali kuzitaka kampuni za simu nchni kujiorodhesha katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) na  kuuza asilimia 25 ya hisa zake, kampuni tatu za Airtel (ltd), MIC  (LTD) Tigo  na Vodacom Tanzana,  tayari  zimetuma maombi ya kujiandikisha katika soko hilo.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, afisa masoko mwandamizi  wa DSE, Mery Kinabo, alisema kampuni hizo  zitaanza kuuza hisa zake mwaka huu 2017 na watanzania  wanakaribishwa kununua hisa hizo pindi zitakapo anza kuuzwa ili kujiongezea kipato na kumiliki uchumi.

Mwishoni mwa mwaka jana, Waziri wa  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa,  alisisitiza kuwa Kampuni zitakazokiuka sheria hiyo zitachukuliwa hatua za kisheria kupitia kifungu cha 21 (C) cha sheria ya EPOCA ya mwaka 2010.

Aidha, aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo kununua hisa hizo na kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni za Mawasiliano nchini ili kujiongeza kipato na kushiriki katika maamuzi ya kampuni hizo.

Pamoja ana hayo Kinabo alizitaja Kampuni tano ambazo ziliongoza kupanda kwa bei ya hisa zake katika soko la hisa la DSE kuwa ni ACA, KA, NMB, TOL na JHL.

“Mwaka 2016 tulipata kampuni tatu ambazo ziliorodhesha hisa zake katika soko la hisa la Dar es salaam ambazo ni Yetu Microfinance, Mufindi Community Bank -MUCOBA Bank na Dar es Salaam Stock Exchange PLC (DSE). Na kampuni mbili ambazo ziliorodhesha hati fungani zake katika soko la hisa ni EXIM Bank LTD na National Microfinance Bank Plc- NMB Bank'' alitanabaisha Kinabo.

No comments:

Powered by Blogger.