LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Kwamba tarehe 4 /1/ 2017 majira ya saa sita usiku (00:00) katika maeneo ya kijiji cha Nyabutanga kata ya Bukokwa tarafa ya Buchosa wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza, askari walifanikiwa kuwakamata watu watano ambao ni;

1. Julius Ndalo miaka 80, 2. George Julius miaka 22, 3. Joseph Julius miaka 28, 4. Mabula Julius miaka 17, na 5. Tabu Dawa miaka 34 wote wakazi wa kijiji cha Nyabutanga, kwa kosa la kujihusisha na kilimo cha bangi kitendo ambacho ni kinyume na sheria, ambapo jumla ya miche ya bhangi 17, 794 iliweza kupatikana katika mashamba yao.
Awali askari walipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya uwepo wa watu wanaojihusisha na kilimo cha bhangi katika kijiji cha Nyabutanga, ndipo majira tajwa hapo juu askari walikwenda maeneo ya mashamba yaliyopo kijijini hapo  na kukuta mashamba mawili yenye ukubwa wa ekari tatu yakiwa yamepandwa bangi pamoja na mahindi. 

Askari walifanya operesheni usiku huo ya kung’oa miche yote ya bhangi katika mashamba hayo, ambapo kiasi cha miche 17,794 ya bangi ilipatikana na kufanikiwa kuwakamata watu watano tajwa hapo juu ambao wanadaiwa kumiliki  mashamba hayo.

Watuhumiwa wapo katika mahojiano na jeshi la polisi, pindi uchunguzi ukikamilika hapo baadae watafikishwa mahakamani, upelelezi na misako ya kutafuta watu wengine ambao wanajihusisha na kilimo haramu cha bhangi bado unaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa Mwanza akiwataka kuacha tabia ya kujihusisha na shughuli zisizo halali ambazo zinakwenda kinyume na sheria na taratibu za nchi, bali wafanye kazi halali, lakini pia anaendelea kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili liweza kudhibiti uhalifu katika mkoa wetu wa mwanza.

Imetolewa na:
DCP: Ahmed Msangi 
Kamanda wa Polisi (M) Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.