LIVE STREAM ADS

Header Ads

UJIO WA NYANZA FESTIVAL 2017 JIJINI MWANZA WAPAMBA MOTO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Kikao cha maandalizi cha Tamasha kubwa la Nyanza Festival kikifanyika Jijini Mwanza, kikiongozwa. Ni tamasha litakalowahusisha wanamuziki mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya.
Picha na Nyanza Festival 2017
Mkurugenzi wa kampuni ya Famara Entertainment, Fabian Fanuel (mwenye kofia) na wajumbe wengine wakiwa kwenye kikao cha maandalizi ya tamasha la Nyanza Festival 2017
Wanakamati wa Nyanza Festival wakipitia miswada mbalimbali ili kufanikisha tamasha hilo mapema mwaka huu
Wanakamati wa Tamasha kubwa la Nyanza Festival 2017
Kikao cha wanakamati kikiendelea Jijini Mwanza
Picha ya pamoja ya baadhi ya wanakamati wa tamasha kubwa la "Nyanza Festival 2017".
Na Binagi Media Group
Nyanza Festival 2017 ni tamasha kubwa la muziki wa kizazi kipya linatorajariwa kufanyika kwa mara ya kwanza Jijini Mwanza na baadaye kusambaa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, Tanzania na nje ya Tanzania.

Ni wazo ambalo lilitoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Famara Entertainment ya Jijini Mwanza, Fabian Fanuel na kupokelewa vyema na wadau wote wa muziki mkoani Mwanza wakiwemo watangazaji, waandishi wa habari, wanamuziki, Madjz, wamiliki wa mitandao ya kijamii (blogs), watayarishaji wa muziki na wengine wengi.

"Tamasha hili litaongeza chachu ya kuikuza sanaa ya muziki ikizingatiwa kwamba upele umepata mkunaji maana linaandaliwa na wahusika wenyewe ambao mara nyingi wamekuwa wakilalamika kukosa fursa ya kutumbuiza kwenye matamasha ambayo yamekuwa yakifanyika". Fanuel ameiambia BMG.

Itakumbukwa kwamba kampuni ya Famara Entertainment kwa miaka miwili mfululizo tangu mwaka juzi, imejijengea heshima kubwa kwa kufanikisha tamasha la dini liitwalo "La Kwetu Concert" katika uwanja wa CCM Kirumba na sehemu ya mapato yake kusaidia wahitaji katika jamii wakiwemo watoto wenye ualibino.

No comments:

Powered by Blogger.