LIVE STREAM ADS

Header Ads

UJUMBE WA PROFESA IBRAHIMU LIPUMBA KWA MAALIMU SEIF.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

James Salvatory, Dar
Mwenyekiti wa Chama cha  Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba amemuomba Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalimu Seif kuendelea na majukumu yake kwani bado anatambulika kwenye nafasi hiyo.

Akizungumza na wandishi wa habari jana katika Maadhimisho ya Siku ya kumbukukumbu ya wanachama wa CUF waliofariki Zanzibar January 26 na 27 mwaka 2001, Profesa Lipumba alisema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, msemaji na kiongozi mkuu wa chama ni Mwenyekiti na moja kati  ya kazi zake ni kumpangia Katibu Mkuu kazi za kufanya na kumuomba.

Alisema anasonoshwa na kuwepo kwa migogoro iyosiokuwa na tija na kuomba kuishimu katiba ya chama hicho na kunapokuwa na matatizo ni bora kuwa na maridhiano na kuwa wepesi wa kisameheana ndani ya chama na kuomba Maalimu Selfu kijirudi Kwa ajiri ya kujenga chama chao

Alisema maadhimisho hayo ni kumbukumbu ya kuwakumbuka wahanga wa maandamano ya amani ya kupinga matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Zanzibar mwaka 2000 yaliyofanyika visiwani Pemba Januari 26 na 27,2001 kuongeza kwamba yalisabaabisha vifo vya watu wapatao 60 hususan wafuasi wa CUF huku watu zaidi ya 2000 wakikimbia makazi yao kutoka Zanzibar hadi Mombasa nchini Kenya.

Alibainisha kwamba CUF imerudi nyuma kisiasa baada ya kupita Uchaguzi Mkuu wa 2015,  kutokana na mgogoro uliosababisha mpasuko wa viongozi wakuu wa chama hicho.

No comments:

Powered by Blogger.