LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAHITIMU WA TOHARA MBADALA WILAYANI TARIME WATAKIWA KUWA MABALOZI WAZURI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Katibu Mkuu Wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba  Nkinga, akihutubia wakati wa mahafali ya tisa katika Kituo cha kuwahifadhi wasichana waliokimbia ukeketaji cha Masanga (ATFGM Masanga), kilichopo Tarime mkoani Mara, ambapo wasichana hao wamehitimu mafunzo mbalimbali ikiwemo kupambana na mila na desturi zenye madhara.
Na Mara Online
Mkuu wa Wilaya ya Tarime (DC) Glorious Luoga, akisisitiza jambo katika mahafali ya tisa ya ATFGM Masanga.  Katikati kushoto kwa DC ni KatibuKatibu Mkuu Wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba  Nkinga  akifuatiwa na Mkrugenzi wa ATFGM Masanga, Stella Mgaya.
Wasichana ambao wamehitumu leo mafunzo ya tohara mbadala katika ushirika wa ATFGM Masanga.
Mangariba wakila kiapo cha kutorudia kukeketa wasichina.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba  Nkinga, amewataka wasichana ambao wamepata mafunzo ya tohara mbadala  katika kituo cha ATFGM Masanga kilichopo Tarime mkoani Mara, kuwa mabalozi wazuri katika kupambana na mila zenye madhara.

“Kuweni mabalozi wazuri katika kuelimisha wasichana wenzenu na wazazi wenu kuwa jambo la muhimu ni kupata elimu”, Sihaba  alisema leo wakati alipokuwa akizungumza  katika mahafali ya tisa ya ATFGM  Masanga katika kijiji cha Masanga.

Katibu Mkuu huyo amesema serikali itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na ushirika wa ATFGM-Masanga.

Aidha  Sihaba amempongeza  Mkuu wa Wilaya  ya Tarime, Glorious Luoga, kwa kazi nzuri anayofanya kuhakikisha tatizo la ukeketaji linaisha katika Wilaya hiyo.

“Tungekuwa na Wakuu wa Wilaya kama Luoga hili suala lingekuwa limeisha", amesema Sihaba.

Katika taarifa  yake fupi, Luoga  amesema mangariba wote ambao wamekeketa watoto wa kike mwaka jana watakamatwa na kufikishwa  mahakamani.

Kwa upande wake Mkurungezi wa ATFGM- Masanga Sr. Stella Mgaya  changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni tabia ya baadhi ya wazazi au walezi kukataa kupokea  watoto wao.

Kwa mujibu wa Sr. Stella ushirika wa ATFGM Masanga umeokoa  zaidi ya wasichana 300 kutofanyiwa vitendo vya ukeketaji musimu uliopita.

No comments:

Powered by Blogger.