LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI WACHACHAMAA NA KUVURUGA KIKAO CHA MAENDELEO YA ELIMU MANISPAA YA ILEMELA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Na James Timber, Mwanza
Baadhi ya wananchi katika Kata ya Bugogwa, Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, wameonekana kukerwa na taarifa zilizotolewa katika kikao cha Maendeleo ya Elimu katika kata hiyo.

Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni diwani wa kata ya Bugogwa, Wiliam Mashambak, aliitisha kikao hicho jana katika viwanja vya shule ya msingi Bugogwa kilichokuwa na lengo la kuchangia suala la elimu katika kuongeza madawati kwenye shule sita za msingi kata hiyo ambazo ni Kabangaja, Igombe, Isanzu, Kilabela, Bugogwa na Kisundi pamoja Shule ya kata ya Sekondari Bugogwa.

Mashamba alieleza kuwa kila kaya inapaswa kuchangia shilingi elfu tano kwa ajili ya utengenezaji wa madawati ambapo kuna kaya 6,000 katika shule za msingi na sekondari.

Hata hivyo wananchi walipinga kauli ya diwani huyo kwa kudai kuwa hakuna kaya 6,000 kwani ni zaidi ya hizo kaya kwa kata nzima na kikao kuvurugika kwa mabishano makali yaliyoibuka.

Diwani huyo alizidi kulaumiwa na wananchi hao wakimtaka aachane na suala la mchango kwanza mpaka atakapowaletea mapato na matumizi ya miradi ya shule hizo ili wawe na uhakika na mchango huo, suala lililopingwa na baadhi ya wanakamati.

Hapo awali halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ilichangia kata hiyo madawati 536 na madawati 139 yakitoka kwa mbunge wa jimbo la Ilemela, Angelina Mabula.

No comments:

Powered by Blogger.