LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAKUU WA MASHIRIKA YA UMEME KUTOKA NCHI KUMI BARANI AFRIKA WAKUTANA JIJINI ARUSHA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Woinde Shizza, Arusha
Wakuu wa  mashirika umeme kutoka katika nchi kumi za Afrika zinazozalisha umeme(Eastern Africa Power pool EAPP)          zimekutana  jijini arusha kwa malengo ya kujadili mfumo wa usafirishaji wa umeme ikiwa ni pamoja na namna wananchi wao watakavyoweza pata nishati ya umeme kwa uraisi tofauti
na sasa.

Hayo yalisemwa na Naibu katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini, Dkt.Juliana Palangyo alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa mashirika ya umeme katika nchi hizo za eastern Africa power pool (EAPP) mapema hii leo.

Palangyo alisema kuwa lengo halisi ni kuweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo nishati ya umeme kwa watumiaji wake kwani  kuna uwezekano  mkubwa wa nchi zote zilizo kwenye umoja huo.
Alisema kwa sasa yapo baadhi ya makampuni ambayo yalikuwa yanauza umeme kwa gharama kubwa hasa kwa wananchi ambao hawajapata huduma hiyo ya umeme lakini kupitia umoja huo wataweza kupata nishati hiyo kwa gharama nafuu.

"Hizi nchi za eastern tumekutana hapa ili tujadili namna ambayo tunaayo wanayoweza kutafuta namna ya kuzalisha umeme kwa bei nafuu na kisha nchi hiyo itaweza kuuza umeme  kwa bei ndogo"aliongeza palangyo.

Hata hivyo kwa upande  kaimu meneja uhusiano wa shirika la tanesco  Leila Muhaji alisema kuwa katika mkutano huo pia watajadili namna ambavyo tanzania itajenga njia ya usafirishaji wa umeme wa njia ya maji ambayo itatoka nchi ya tanzania kwends kenya,zambia,pamoja na nchi nyingine.

Muhaji alisema kuwa tanzania itanufaika na ujenzi wa njia hizo hivyo jamiii itanufaika kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwenye nchi ambazo zimeeendelea duniani.

"Hataivyo mara baada ya huu mkutano wa wakuu wa nchi zinazolisha umeme tunatarajia pia kuwepo na wadau wengine ambao ni mawaziri kutoka nchi zote ambao nao sasa wataweza kuweka mambo sawa ili huduma iweze kumfikia mlengwa". Aliongeza Muhaji.

Alimalizia kwa kutaja nchi ambazo zina unda umoja huo kuwa ni  Tanzania, Kenya,Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan, Dr congo, Ethiopia, Djbout, Libya pamoja na Egypt.

No comments:

Powered by Blogger.