LIVE STREAM ADS

Header Ads

WADAU WAHIMIZWA KUCHANGIA UKARABATI WA UWANJA WA CCM KIRUMBA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, Mwanza
Wadau wa mbalimbali wa michezo mkoni Mwanza, wameombwa kujitokeza kusaidia ukarabati wa miundombinu ya kupitisha majitaka, katika eneo la uwanja wa CCM Kirumba.

Hii ni kutokana na changamoto ya maji kutuama karibu na geti la kuingilia uwanjani hapo na kuwapa usumbufu wapenzi wa soka, wakati wakienda kushuhudia michuano mbalimbali uwanjani hapo.

Wito huo ulitolewa jana na Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba, Steven Shija, wakati akizungumza na BMG ofisini kwake wilayani Ilemela mkoani hapa.

Shija alisema, ukarabati huo unahitaji mifuko 100 ya saruji pamoja na sh.4.2 milioni,ikiwa ni gharama za fundi na vifaa vingine, ili kukamilisha ujenzi huo.

Alisema, kufuatia shughuli za kilimo zilizokua zinaendelea katika eneo la uwanja, zimepelekea kuharibu miundombinu wa mkondo wa kupeleka maji  ziwani,hivyo kufanya maji yanayotiririshwa kukosa muelekeo na kutuama.

Pia alisema, ukarabati huo, utasaidia wanafunzi wa shule ya msingi Kitangiri kutopata usumbufu wakati wa masika.

Hata hivyo alisema, mazingira ya uwanja kwa sasa ni nzuri ikiwemo vyoo,licha ya nyasi kukauka,ila wanafanya jitihada za kupatikana maji mara baada ya mabomba ya maji kupata itilafu na tayari wamewasiliana na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Mwanza   (MWAUWASA),kwa ajili ya matengenezo.

"Kwa sasa uwanja unakabiriwa na ukaukaji wa nyasi,kutokana na shida ya maji baada ya miundombinu ya maji  ambayo imeharibika,hivyo waliwasiliana na MWAUWASA, ili kurekebisha,licha ya kuwa na kisima ambacho akikidhi mahitaji," alisema Shija.

No comments:

Powered by Blogger.