LIVE STREAM ADS

Header Ads

WENJE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CHADEMA KANDA YA ZIWA.


Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekiel Dibogo Wenje (Chadema 2010/15) amechaguliwa kwenye mkutano mkuu wa Kanda ya Ziwa Victoria, kuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda hiyo. 

Wenje alimshinda Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Chief Kalumuna ambapo Uchaguzi huo ulifanyika jana Januari 18,2017 Jijini Mwanza na matokeo kutangazwa majira ya tatu usiku.

Katika uchaguzi huo, nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilichukuliwa na Ansbert Ngurumo ambapo viongozi mbalimbali wa Chadema Taifa akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe, walihudhuria mkutano.
Binagi Media Group

No comments:

Powered by Blogger.