LIVE STREAM ADS

Header Ads

KONGAMANO LA VIJANA WAZALENDO JIJINI MWANZA KUPINGA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA LAFANA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Mratibu wa Kongamano la kujadili namna ya kupambana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya Jijini Mwanza, Denis Kankono, akiteta jambo na Katibu wa UVCCM mkoni Mwanza, Philipo Elieza, kwenye kongamano hilo.
BMG

Vijana wazalendo Jijini Mwanza kupitia taasisi ya Chinga Respect & Complex wameahidi kutumia juhudi zao kuungana mkono jitihada za serikali za kupambana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Hayo yalibainishwa jana na Denis Kankono ambaye ni Mwenyekiti wa kongamano la kujadili namna ya kupambana na biashara pamoja na matumizi ya dawa za kulevya lililoandaliwa na taasisi hiyo Jijini Mwanza.


Alisema vijana ambao ni wahanga wakubwa wa matumizi ya dawa za kulevya nchini wanaowajibu wa kuhakikisha biashara na matumizi ya dawa hizo yanatokomezwa kwani madhara yake ni makubwa katika jamii.



Baadhi ya vijana ambao ni wahanga wa matumiz ya dawa za kulevya Jijini Mwanza waliomba kuendelea kusaidiwa ili kuondokana na matumizi ya dawa hizo ambazo bado upatikanaji wake ni mkubwa licha ya baadhi ya wauzaji kukamatwa na jeshi la polisi. 

Wadau mbalimbali meza kuu
Kulia ni Mwenyekiti wa kongamano hilo, Denis Kankono akiwa pamoja na Katibu wa UVCCM mkoni Mwanza, Philipo Elieza, kwenye kongamano hilo.
Grace Shindika kutoka UWT Wilayani Nyamagana akiwasilisha mchango wake katika kupambana na biashara na dawa za kulevya
Mdau kutoka kundi la machinga akiwasilisha mchango wake
Mmoja wa vijana wazalendo Jijini Mwanza akiuliza swali pamoja na kuwahamasisha vijana wenzie kuepukana na matumizi ya dawa za kulevya
Mmoja wa vijana kutoka Chuo cha Saut Mwanza akiuliza swali
Mmoja wa wachangia mada kutoka Chuo cha Saut Mwanza akitoa mchango wake wa mawazo ili kupambana na dawa za kulevya
Washiriki wa kongamano hilo
Zaidi ya vijana wa kike na kiume 30 kutoka Jijini Mwanza ambao ni wahanga wa matumizi ya dawa za kulevya na wenye nia njema ya kuachana na kadhia hiyo walishiriki kongamano hilo.

No comments:

Powered by Blogger.