LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MISUNGWI ATETA NA WADAU WA KILIMO NA UVUVI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Timber,  Misungwi       
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Eliud Mwaiteleke (pichani), amewataka wadau wa  kilimo na Uvuvi kutumia vyema fursa za Maendeleo ya  Sekta ya Kilimo na Mifugo zinazotolewa na taasisi za umma zilizopo wilayani hapo.


Mwaiteleke alisema hayo wakati wa ziara katika  Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiriguru, Chuo cha Mafunzo ya Kilimo Ukiriguru, Shamba la Uzalishaji wa Mifugo la Mabuki, Kituo cha Utafiti wa Mifugo Mabuki pamoja na Chuo cha Mafunzo ya Mifugo Mabuki.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Habari na Mawasiliano katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Thomas Lutego alieleza   vipaumbele vya halmashauri katika juhudi za kukuza uchumi  ambapo ni pamoja kufufua kilimo cha zao la pamba na kuanzisha  kilimo cha zao la alizeti ikiwa ni zao la biashara pamoja na kusindika mafuta yatokanayo na zao hilo.


Lutego alisema kuwa halmahsuri itatoa  mbegu za alizeti kwa kuwakopesha wakulima, ambapo tayari Maafisa Ugani na Watendaji wa Kata na Vijiji wanaendelea na utoaji wa elimu kwa wakulima na kuwaorodhesha ili kupata takwimu halisi ya mahitaji kwa msimu huu.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Ukiriguru, Everine Lukonge alisema wameweza kubaini vipengele mbalimbali vya kuongeza thamani ya mazao ikiwemo zao la pamba,  mihogo, ulezi, mtama, mbaazi, dengu, karanga na alizeti ambapo yanafaa kwa asili ya udongo katika Wilaya ya hiyo.


Lukonge alisema kwamba  vijiji vilivyofanyiwa utafiti na kufanikiwa kulima vizuri katika zao la dengu katika  Kijiji cha Iteja na Ilalambogo, mtama na uwele na kulimwa katika Vijiji vya Ng’ombe na Mapilinga.

No comments:

Powered by Blogger.