LIVE STREAM ADS

Header Ads

TANZANIA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MSUMBIJI BAADA YA WASIO NA VIBALI KUTIMULIWA NCHINI HUMO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

James Salvatory, Dar
Waziri wa Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Augustino Mahiga amesema oparesheni inayofanyika Msumbiji ya kufukuza raia wakigeni waliyoingia nchini humo bila kufuata taratibu za kisheria bado mazungumzo kati ya Idara za uhamiaji za Serikali ya Tanzania na Msumbiji yanaendelea.

Hayo ameyasema leo Jijini Dar es salaam wakati akijibu maswali ya wanahabari  wakati wa mkutano wake na wanahabari ,uliyokuwa na malengo ya kutoa taarifa kwa umma juu ya Ujio wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ambaye anatarajiwa kuwasili hapa nchini  februari 25 mwaka huu, kwa ziara ya siku 2 ya kutembelea shughuli mbalimbali za Maendeleo pamoja na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake Rais John Magufuli.

Mahiga amesema kuwa raia wengi ambao wamekuwa wakiingia Msumbiji wamekuwa wakijihusisha na shughuli mbalimbali kinyume cha sheria ikiwemo kutafuta Ajira  bila kibali cha kufanyia kazi ndani ya nchi hiyo.

Aidha ameongeza  kuwa wengine wanajihusisha na uuzaji wa Silaha,Madawa haramu ya Kulevya pamoja na ukwapuaji wa mali za watu,hivyo kufuatia vitendo hivyo Serikali ya Msumbiji imeamua kufanya oparesheni ya kufukuza raia wote wa kigeni waliyoingia ndani ya Taifa hilo kinyume cha sheria.

Hata hivyo amesema kuwa kesho kutakuwa na mkutano wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika( SADC) ambao utafanyika jijini Dar es salaam kuanzia majira ya saa tatu asubuhi,ambapo suala la oparesheni ya kuwaondoa  raia wa kigeni nchini Msumbiji nakusababisha baadhi kupoteza maisha na wengine mali zao,  itakua ni moja ya ajenda zitakazojadiliwa.

Watanzania waliyofukuzwa Msumbiji hadi sasa inasemekana kufikia kiasi ya watu,na wamekuwa wakipokelewa katika ofisi za uhamiaji Mkoani Mtwara na Kupelekwa katika mikoa wanayotoka hapa nchini. 

No comments:

Powered by Blogger.