UONGOZI WA UWANJA WA CCM KIRUMBA WATOA SHUKURANI KWA WADAU WA MICHEZO MWANZA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
" Tunaendelea kuamini kuwa kazi hii haitakuwa nyepesi kama
wadau hawataweza kujitokeza na kujitolea kwa hali na mali, hivyo
tunaomba ushirikiano wenu ili kukamilisha ujenzi huu," alisema Shija.
Judith Ferdinand, Mwanza
Uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba unawashukuru wadau wa
michezo mkoani hapa, waliojitolea kuchangia vifaa vya ujenzi hususani
saruji pamoja na uchimbaji wa mkondo wa kupitisha maji taka.
Hii ni baada ya mkondo huo kuharibiwa na shughuli za kilimo
zilizokuwa zinafanyika katika eneo la uwanja huo na kusababisha maji
kutuama karibu na lango la kuingilia uwanjani na kuwa kero kwa mashabiki
wanaoenda kushuhudia michuano mbalimbali pamoja na wanafunzi wa shule
ya msingi Kitangiri hasa kipindi cha masika.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Meneja wa Uwanja huo Steven
Shija wakati akizungumza na BMG ofisini kwake wilayani Ilemela mkoani
Mwanza.
"Tunamshukuru Mungu na wadau walijitolea kuchangia ujenzi
huu wa ukarabati wa mkondo wa kupitisha maji taka, kwani hatua ya awali
ya uchimbaji umekamilika kwa asilimia 95 na asilimia 5, iliyobaki ni
mifereji ya pembeni inayochepukia kwenye mfereji mkuu, hivyo tunaenda
hatua ya ujenzi ambayo imegawanyika katika hatua mbili," alisema Shija.
Shija alisema,hatua ya kwanza ni ujenzi wa daraja na sehemu
ya kupokelea maji kuyaelekeza kwenye mkondo mkubwa, hii itasaidia
kuzuia maji yasiingie shule ya msingi Kitangiri.
Pia alisema, vifaa vinavyotakiwa kukamilisha daraja ambalo
ndio hatua ya kwanza ya ujenzi huo ni nondo 20(Mm12), kokoto tripu 2,
mchanga tripu 2, mbao 20(1×8), BRC 6 mita, mawe tripu 4 na gharama za
kulipa mafundi, kwani kwa sasa wanafunzi na wananchi wanavuka kwa tabu
kwenye mtaro huo.
Hata hivyo alisema,hatua ya pili ni kujenga mkondo wa maji
sehemu iliyobaki yenye mita 185, ambayo mahitaji yake yatatajwa baada
ya kukamilisha hatua ya kwanza ambayo ni muhimu kwa sasa, pia saruji za
kuanzia kazi wanazo.
No comments: