LIVE STREAM ADS

Header Ads

FANYA HAYA ILI UWE MPYA MAISHANI MWAKO.

Ibada za leo Jumapili, Machi 05, 2017, kanisa la EAGT Lumala Mpya, Jijini Mwanza.

Somo:
Kwa nini tuwe wapya (Uwe Mpya)?.
Mchungaji:
Dkt.Daniel Moses Kulola.

Rejea maandiko hapo chini:
2-Wakoritho 5:20
2-Wakoritho 5:17
2-Wakoritho 521
Isaya 40:31
Maombolezo 3:23
Ezekiel 36:26

Mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya. Ya kale yote yamepita. Ukiokoka unakuwa mpya kwa sababu umempokea Yesu Kristo.

Ukiokoka, Yesu anashughulika na maisha yako. Kupitia Yesu, Mwenyezi Mungu anakuwa anashughulika kukuondolea vitu visivyofaa maishani mwako.

Ukiwa ndani ya Kristo, Yesu anapambana na watesi wako, na kamwe hawawezi kukushinda maana umekuwa mpya. Atapambana na wagomvi wako, magonjwa yako na kila aina ya mateso mbele yako.

Lakini yakupasa ukiokoka, uenende katika matendo mema ili Yesu aendelee kukaa ndani yako na kuihuisha dhambi yako (ya mwanadamu) ya asili ili uendelee kupata kibali zaidi mbele za Mungu.

Ukiokoka unakuwa ndani ya Kristo hivyo usikosee ukatoka maana ni rahisi shetani kukushambulia.

Mungu anasema, anza upya, ukiisha kubali kuokoka/ kuwa mpya. Kama ulikuwa ukitenda dhambi hata kwa kificho ikiwemo ulevi, acha na ishi maisha ya wokovu ili uendekee kukubalika katika ukuu wa Mungu.

Kumbuka Yesu alibeba dhambi zetu zote ili alete upatanisho kati yetu (mwanadamu) na Mungu. Alisurubiwa Yesu kwa ajili ya mwanadamu. Ya kale yote yakapita na wote waliompokea wakawa wapya.

Hakika zipo sababu za kujiuliza, kwa nini uwe mpya. Utakuwa mpya ikiwa utaokoka/ umeokoka na kuyaacha ya kale yote ikiwemo ulevi, uzinzi, uchawi, wizi, uongo na kila aina ya uovu maishani mwako.

Na kamwe usisahau kila siku kumuomba Mungu ili akufanye kuwa mpya maishani mwako. Shughuli, biashara, kazi, ndoa na mambo yako maishani, vyote viwe vipya.

Kuwa na tafakuri njema, ndimi George Binagi.
Fuatilia mafundisho zaidi kupitia eagtlumalampya.blogspot.com ama binagimediagroup.blogspot.com na Mungu akubariki.

No comments:

Powered by Blogger.