LIVE STREAM ADS

Header Ads

LESENI YA MGODI WA BUCKREEF MKOANI GEITA KUCHUNGUZWA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mwenyekiti wa kamati  ya Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko,akizungumza wakati wa kikao cha tathmini juu ya maeneo na migodi ambayo wamezungukia Mkoani Geita.

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Mara Joyce  Sokombi akiandika baadhi ya point zilizokuwa zikizungumzwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo.

Wajumbe wakifuatilia Kikao.

Mwenyekiti wa kamati  ya Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko,akitoa maagizo kwa wanufaika wa Ruzuku.
Kaimu Kamishna wa Madini ,Mhandisi Ally Samaje akimwakikishia Mwenyekiti wa kamati hiyo kutekeleza maagizo  ambayo ameyatoa.
Naibu Katibu Mkuu Prof,James Mdoe,akisisitiza   kwa wachimbaji  ambao wamepatiwa Ruzuku  mpango wa kuwazungukia wote. Mwenyekiti wa halamshauri ya Mji wa Geita,Lernad Kiganga Bugomola akijitambulisha kwa wajumbe.

Meneja Mahusiano ya jamii mgodi wa GGM ,Manase Ndoloma akielezea namna mgodi huo umekuwa ukichochea maendeleo kwa wananchi Mkoani Geita.Kamati ya  Bunge ya Nishati na Madini imeitaka wizara hiyo  na Stamico  kuangalia ubia na leseni  ya mgodi wa Buckreef Gold Company Limited uliopo  Rwamgasa ambao kwa muda umekuwa ufanyi kazi za uchimbaji   huku kuna wachimbaji wadogo wamekuwa wakihitaji kufanya shughuli za uchimbaji  kwenye maeneo ambayo yameshikiliwa na mwekezaji .

Akizungumza baada ya ziara ya siku nne Mkoani Geita,Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko,amesikitishwa na mwekezaji wa Backreef kushikilia eneo kubwa huku kuna baadhi ya wananchi wanaidai kampuni hiyo fedha nyingi.

“Kuna eneo la Backreef  tunakuomba sana na tunaitaka Wizara na Stamico muende mfanye haraka sana muangalie patna ship zenu  mnaleta wabia ambao kwa sehemu kubwa ni wajanja wajanja tu hakuna wanachofanya eneo wamelikalia  wachimbaji wadogo wadogo mngewapatia eneo hilo ingekuwa na maana kubwa zaidi kuliko mnampatia mtu mmoja mgeni anashika eneo kubwa leseni 13 kwa miaka yote hakuna anacho fanya halafu tunaona sisi watanzania tumezidiwa akili na mtu mmoja hilo halikubaliki lakini msimamie kuna madeni ambayo watanzania wanamdai ahakikishe anayalipa”Alisema Biteko.

Sanjari na hayo Mwenyekiti Biteko,ameitaka wizara kuhakikisha fedha za ruzuku zinawafikia walengwa na kwamba pesa hizo zisipelekwe kwenye matumizi ambayo ni kinyume na shughuliza za uchimbaji.

Hata hivyo kwa upande wake  Kaimu Kamishna wa Madini ,Mhandisi Ally Samaje amemwakikishia Mwenyekiti wa kamati hiyo kutekeleza maagizo ya kamati ikiwa ni pamoja na fedha za ruzuku kufanya kazi ambazo  zinatakiwa.


Naibu Katibu Mkuu Prof,James Mdoe,amesisitiza kuwa kwa wachimbaji  ambao wamepatiwa Ruzuku kuna mpango wa kuwazungukia wote na kujua namna ambavyo wametumia fedha hizo na kwamba hoja zote zilizozungumza watazijibu kwa maandishi kujua maamuzi ambayo wameyachukua kutokana na fedha za ruzuku.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE 

No comments:

Powered by Blogger.