LIVE STREAM ADS

Header Ads

TANZANIA KUJADILI TAFITI ZA MABADILIKO YA KIUCHUMI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Na James Salvatory, Dar
Tanzania imejipanga kujadili kwa pamoja matokeo ya tafiti   zilizofanyika nchini na  nchi nyingine, lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu na nchi nyingine ili kuwezesha mabadiliko ya kiuchumi na kusukuma maendeleo ya viwanda.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayoshujighulisha na utafiti kuhusu kupunguza umaskini  (REPOA,)  Dr.Donald Mmari, amesema kuwa mikakati ya serikali ni kufikia uchumi wa  kati mpaka 2025 na sekta ya viwanda hasa vya kati ni sekta ambayo inajumuisha watu wengi na kama nchi ikiweza kuwa na viwanda vya uwezo wa  kati itaweza kuwasaidia wananchi wengi ambao hawaitaji kuwa na taaluma kubwa hivyo kusaidia uchumi kukuzwa na watu wa kawaida

Aidha amesema kuwa  tasisi hiyo imekuwa ikifanya mikutano kila mwaka ambao huwa inajumuisha wadau mbali mbali,watafiti, wanataaluma,wadau wa maendeleo pamoja na watunga Sera na mkutano wa mwaka huu utakuwa wa 22 ikiwa nmada  kuu ni kuangalia masuala ya viwanda ili kuweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini.

Kwa upande wake Mtafiti Mwandamizi, Dr. Brandina Kilama amesema ni vema kuwepo kwa sera ambazo zina mikakati ya kufanya kazi ambayo itaziwezesha taasisi kufanikisha kufikia uchumi wa kati mwaka 2025.

No comments:

Powered by Blogger.